Jumatano, 29 Juni 2011

VIGOGO ARDHI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Wednesday, June 29, 2011 12:10 PMVIGOGO nane wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi wakiwemo na Maofisa wa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kutumia madaraka wakwia kazini
Vigogo hao walifikishwa jana katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni kwa
kosa la kuruhusu viwanja vya wazi vilivyopo ndani ya Manispaa hiyo kuvamiwa hali wakiwa kazini.

Mbele ya Hakimu Yohana Yongolo wa Mahakama hiyo watuhumiwa hao walisomewa mashitaka tofauti yaliyofikia 44 yote yakiwa kutumia madaraka vibaya.

Waliofikishwa mahakamanai akiwemo Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Hamidu Mgaya, Anna Macha na Mapambano Baseka
Maofisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi waliofikishwa mahakamani hapo ni Said Maligwah, Jumla Mmalala, Francis Woiso na Wanura Maranda.

Vilevile aliyekwua diwani wa Kata ya Kunduchi [ccm] Patrick Matoyola

Vigogo hao wamefikishwa mahakamani ikiwa ni ahadi ya Waziri ya husika kuwawajibisha wale wote waliohusika na kuza viwanja vya wazi ikiwa na wale wote waliosababisha uvamizi

Jumanne, 28 Juni 2011

PICHA YA LEO; MAREHEMU RAIS CHILUBA NA MKEWE, PAMOJA NA MISUKOSUKO YA SHUTUMA ZA RUSHWA,BADO ANABAKIA BABA WA MAGEUZI YA VYAMA VINGI ZAMBIA NA AFRIKA PIA. R IP

Chiluba na mkewe enzi za uhai wake,kazikwa juzi.

MAHAKAMA YA KIMATAIFA YATOA HATI YA KUKAMATWA GADDAFFI, IS IT A FAIR COURT OF LAW!?

Waziri wa sheria nchini Libya Mohammed al Qamoodi amesema hati za mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita za kutaka Kanali Muammar Gaddafi akamatwe zimelenga kuficha uhalifu wa Nato.
Kanali Muammar Gaddafi


Akizungumza mjini Tripoli, Bw Qamoodi amesema operesheni za Nato zinazoendelea nchini humo ni uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Libya lakini ICC imezifungia jicho.
Waziri huyo ameongeza kuwa wanajeshi wa Nato sasa wamepata kisingizio cha kumuua kiongozi wao Kanali Gaddafi.
Hata hivyo ametangaza kuwa Libya imepata fursa ya kufungulia Nato mashtaka ya uhalifu wanaoendeleza nchini Libya.
Mahakama hiyo imemtuhumu Gaddafi kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.
Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa idara ya ujasusi Abdullah al-Sanussi.
Hatua hio imeendelea kuzua hisia tofauti.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Urusi, Konstatin Kosachev amesema kuwa uamuzi wa jaji hao sasa utavuruga juhudi za kutafuta suluhu ya mzozo huo.
Bw Kosachev amesema nia kuu ya jumuiya ya kimtaifa ni kuwa Kanali Gaddafi ajiuzulu na atoke nchini humo lakini sasa hilo huenda lisifanyike.
Badala yake, Kosachev amesema huenda kiongozi huyo atafanya kila juhudi kushinda vita hivyo na hii sio habari njema kwa Libya.
Lakini kwa upande wao, wapinzani wamekaribisha uamuzi huo.
Msemaji wao Ibrahim Dabbashi amesema sasa jukumu lipo kwa washirika wa Gaddafi kuelewa kuwa wanafanya kazi na mhalifu na wamshauri aondoke madarakani.
Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.

WALOKAMATWA NA MAMILIONI YA DOLA SOMALIA WAACHIWA

..Wabeba kikombozi wasamehewa
Wakuu wa Somalia wamewasamehe wageni 6 waliokutikana na hatia ya kuingiza nchini dola milioni-tatu, ili kuwalipa maharamia kikombozi.

Harmia la kisomali


Msemaji wa serikali ya mpito, Abdirahman Osman Yarisow alieleza wanaume hao, kutoka Uingereza, Marekani na Kenya waliachiliwa huru kwa sababu ya kuwaonea huruma.

Alisema kikombozi walichokuja nacho kimetaifishwa na serikali.

Juma lilopita, wanaume hao walihukumiwa kifungo cha miaka 15.

Washtakiwa hao walikamatwa mwezi uliopita punde baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege mjini Mogadishu.

Watu hao walifanyiwa kesi ya faragha kwenye uwanja wa ndege ambako walitua mwezi uliopita.

Inasemekana walipowasili Mogadishu walikuwa wamebeba mamilioni ya dola kama kikombozi.

Msimamo rasmi wa serikali ya Somalia ni kuwa inapinga kulipa kikombozi lakini tabia hiyo imekuwa ni kawaida sasa.

Umoja wa mataifa unakisia zaidi ya dola milioni moja zililipwa kwa maharamia wa Somalia mwaka jana

OCEAN VIEW MAMBO SAFI KAGAME CUP


Timu ya Ocean view ya Zanzibar imejiwekea mazingira mazuri zaidi ya kufuzu robo fainali ya michuano ya Kombe Kagame baada ya kuifunga Red Sea ya Eritrea mabao 2-0.

Kutokana na ushindi wa mchezo huo uliofanyika mchana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Ocean View imefikisha pointi sita na kuongoza kundi hilo, baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Etincelles ya Rwanda mabao 3-2.

Ocean View sasa imebakisha michezo miwili wa kwanza itacheza na Simba kesho na mwingine itaumana na Vital ‘O ya Burundi Jumapili.

Kihesabu inaweza kuonekana kana kwamba tayari Ocean View imefuzu kwa vile timu zinazotakiwa kufuzu robo fainali kwa Kundi A ni tatu, lakini kisoka bado kwa vile inaweza kupoteza michezo yake yote iliyobaki, kisha wapinzani wake wakashinda michezo yao hivyo kupita pointi sita ama kuwa sawa na badala yake idadi ya uwiano wa mabao ukaamua.

Katika mchezo wa jana, Ocean View ilipata bao la kwanza dakika ya 35 mfungaji akiwa Haji Suleiman kutokana na pasi ya Mohammed Hamduni.

Red Sea licha ya kufungwa mchezo huo ilipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji haukuwa mzuri, ambapo itajutia zaidi nafasi iliyopata dakika ya 16 wakati Abraham Tedros alipoingia ndani ya eneo la hatari, lakini shuti lake lilipanguliwa na kuwa kona butu.

Red Sea ililazimika kucheza pungufu dakika ya 77 baada ya Aron Zekarias kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Salum Shebe.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, ambapo dakika ya 86 Said Rashid alifunga bao la pili kwa shuti lililoenda moja kwa moja wavuni.

Kulingana na taratibu za Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), timu tatu za Kundi A, pamoja na timu mbili za juu Kundi B na mbili za Kundi C zitacheza robo fainali pamoja na timu itakayokuwa na uwiano mzuri wa pointi kutoka Kundi B ama C.

Katika mchezo mwingine uliofanyika jioni kwenye uwanja huo timu ya Vital ‘O ya Burundi ambayo mchezo wa kwanza ilitoka 0-0 na Simba iliifunga Etincelles ya Rwanda mabao 3-1
Mabao ya washindi yalifungwa na Nzigamasabo Steive, Minzi Stanley na Mbakiye Babi wakati la Etincelles lilifungwa na Ochaya Sylvan.

Vital’O sasa imefikisha pointi nne kwa michezo miwili. Michuano hiyo inaendelea tena leo kwa mchezo wa Kundi B, ambapo Bunamwaya ya Uganda itacheza na Elman ya Somalia

Jumatatu, 27 Juni 2011

EL MEREIKH YAILAZIMISHA SULUHU YANGA

BAO tata lililofungwa dakika ya 63 na Stephen Worgu jana lilifanya mchezo wa Yanga na El Merreikh ya Sudani umalizike kwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Kundi B la michuano ya Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Worgu alifunga bao hilo kwa mpira ulionekana kama umegonga mwamba na haukuvuka mstari wa goli, lakini mwamuzi Mganda Dennis Batte akiashiria mpira uendelee.

Wakati huo Yanga ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1, huku wachezaji wa El Mereikh ya Sudani wakinyoosha mikono kulalamika kwamba mpira ulivuka mstari wa goli, kabla ya kipa Yaw Beko kuokoa.

Sekunde chache baadaye mwamuzi msadizi Simba Honore wa Rwanda alinyoosha kibendera juu kumpa ishara Batte kwamba mpira ulivuka mstari na kwamba lilikuwa bao, hivyo Batte kuashiria mpira uwekwe kati.

Ukiacha bao hilo, mchezo wa jana ulikuwa wa ushindani karibu dakika zote 90, huku Yanga ikitawala kipindi cha kwanza na wageni kudhibiti kipindi cha pili.

Yanga ilipata nafasi nyingi za kufunga kipindi cha kwanza, lakini Kenneth Asamoah, Davies Mwape, Julius Mrope na Rashid Gumbo kwa nyakati tofauti walishindwa kuzitumia.

El Merreikh nayo ilipata nafasi nyingi za kufunga, lakini mashuti ya washambuliaji wake ama yalishindwa kulenga lango ama yaliokolewa na kipa Berko.

Wachezaji Kelechi Osunwa, Wawa Pascal, Remi Adiko walikuwa wakiisumbua ngome ya Yanga lakini umaliziaji ulikuwa butu.

Katika mchezo huo Merreikh ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya pili mfungaji akiwa Osunwa kwa kichwa, kabla ya Yanga kusawazisha dakika tano baadaye baada ya beki Ahmed Albasha wa Merreikh kujifunga baada ya kumrudishia mpira uliomshinda kipa wake Isam Elhadari.

Yanga iliongeza mashambulizi na kupata bao la pili dakika ya 35 mfungaji akiwa Kenneth Asamoah.

Juzi wawakilishi wengine wa Tanzania Bara katika michuano hiyo Simba, ilitoka 0-0 na Vital ‘O ya Burundi mchezo wa Kundi A.

Yanga: Yaw Berko, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub, Nurdin Bakari, Julius Mrope, Rashid Gumbo, Davies Mwape, Jerry Tegete/Kenneth Asamoah, Kigi Makasi.

El Merreikh: Isam Elkhadari (Gk), Saeed Mustapha, Badr Eldin, Ahmed Albasha, Nasr Eldin, Musab Omer, Kelechi Osunwa, Balla Gabir, Wawa Paschal, Karim Eddaffi na Remi Adiko.

Wakati huohuo, John Nditi anaripoti kutoka Morogoro kuwa timu ya APR ya Rwanda jana iliifunga Ports ya Djibouti mabao 4-0 mchezo uliofanyika Uwanja wa Jamhuri.

Mabao ya APR ambao ni mabingwa watetezi yalifungwa na Nyirenda Victor aliyefunga mawili, Logbo Landry na Kwizera Ernest
Monday, 27 June 2011
Waziri wa NIshati na Madini William Ngeleja akiwa bungeni, jana wabunge walimshutumu kuwa tokea ateuliwa katika nafasi yake hakuna alichokifanya katika wizara yake

Kizitto Noya na Habel Chidawali, Dodoma
WABUNGE wameibana Serikali na Shirika la Umeme nchini(Tanesco), wakitaka majibu ya kina kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuhusu ukiritimba wa shirika hilo la umma, mikataba mibovu, mgawo wa nishati ya umeme na bei yake.

Hayo yalitokea jana mjini hapa wakati wa semina iliyoandaliwa na Ngeleja kwa wabunge hao kuhusu uendeshaji wa sekta ya umeme nchini.

Wabunge waliochangia mjadala huo walionyesha kukerwa na huduma mbovu za Tanesco wakieleza kuwa haziridhishi huku baadhi yao wakilalamikia bei kubwa ya umeme.

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene alimjia juu Ngeleja na kueleza kuwa ndiye chanzo cha tatizo hilo kwa kuwa sera na mipango yake havitekelezeki.

“Kila mwaka unakuja na mipango hiyo hiyo, naweza kusema kuwa tangu Ngeleja uwe waziri, hujatusogeza hata hatua moja,”alisema.

Aliongeza:“Ngeleja huna jambo lolote ambalo umelifanya tangu ulipoingia katika wizara hii, kila siku ni michakato ambayo haina majibu. Watanzania wanataka umeme siyo porojo, acheni porojo za makabrasha ya karatasi.’’

Simbachawene, ambaye pia ni mwenyekiti wa Bunge alimwambia Waziri Ngeleja kuwa taifa linataka umeme na siyo mipango isiyotekelezeka ambayo haiwasaidii kuwaondolea umaskini wananchi

Naye Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) aliitaka Serikali ieleze kwa nini mitambo ya Dowans iliyozua mjadala mzito nje na ndani ya Bunge kutokana na kile kilichoelezwa kukosa ubora sasa inaendelea kutumika.

“Mimi nashindwa kuelewa, hivi tatizo kwenye mitambo ya Dowans ilikuwa nini? Maana tulielezwa kuwa ni mibovu na haina viwango, lakini hivi juzi alikuja Mwarabu akazungumza na Rais (Jakaya Kikwete) na sasa tunaambiwa kuwa mitambo hiyo ni bora sana…tatizo ilikuwa kweli mitambo au mtu, nataka majibu”alieleza.

Juma Nkamia, ambaye ni Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), alihoji mantiki ya bomba la gesi kutandazwa kutoka Mtwara hadi Tanga wakati kuna maeneo mengi njiani ikiwamo Kanda ya Kati, ambayo hayana nishati hiyo ya gesi au hata umeme.

“Kwa nini bomba litoke Mtwara lipite Dar es Salaam mpaka Tanga? Hivi Kanda ya Kati mnaionaje? Kwa nini lisipite huku? Hivi ni kwa sababu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco (William Mhando) anatoka Tanga au kwa sababu Makamba (Januari) , ambaye ni Mwenye,kiti wa Kamati ya Bunge ya Nishatianatoka huko?”alihoji.

Baada ya kauli hiyo, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage alisimama na kuomba taarifa, kisha akasema, “Sio sahihi kusema hivyo kwani Makamba na Mhando ni watekelezaji tu wa mipango siyo wapangaji. “

Mwenyekiti wa semina hiyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Diana Chilolo alikazia hoja ya Mwijage akisema, "Utungaji wa sera unaanzia kwenye wizara na baadaye inakuja Baraza la Mawaziri na mwisho kwenye Kamati za Bunge.

Kamati ina wajumbe 27 na Makamba hawezi kuwaburuza wenzake 26,”alisema Chilolo na kuongeza:

“Na mimi ni mwanamke, mbunge kwa miaka 15 sasa. Siwezi kuburuzwa na mtu mmoja.”

Baadaye, Nkamia aliilipua Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (Ewura), akisema ni taasisi inayotumia vibaya fedha za umma kwa kulipana posho za vikao huku ikiwa haina utendaji uliotukuka.

“Posho ya ofisa wa Ewura kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni kubwa kuliko nauli ya mbunge kwenda Marekani. Mimi nimewahi kuwa mwandishi wa habari na mara kadhaa tumekuwa tukisikia Ewura wamekamata mafuta yaliyokuwa chini ya viwango. Hebu leo watuambie mafuta hayo huwa wanayapeleka wapi?”Alihoji.

Katika mchango wake, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi) alipinga mpango wa Tanesco wa kupeleka umeme wa uhakika mkoani Kigoma mwaka 2016 akisema ni mbali mno na hiyo itaathiri mradi wa kutengeza saruji uliopangwa kuanza mkoani humo.

Alisema katika kipindi kifupi alipatikana mwekezaji kutoka Marekani, lakini alishindwa kuwekeza katika kiwanda ambacho kingezalisha saruji kwa wingi na kufanya bei ya bidhaa hiyo kupungua kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, mbunge huyo aliwataka Tanesco kutafuta fedha hata kama ni kwa kukopa, ili kutimiza malengo yao na kwamba fedha hizo zitaingia katika utaratibu wa tozo kupitia makampuni ya simu za mikononi.

Kafulila alisema kulingana na idadi kubwa ya Watanzania wanaotumia simu za mikononi, deni hilo linaweza kulipwa ndani ya miaka mitatu.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) alitaja chanzo cha kukwama kwa maendeleo ya Tanesco kuwa ni mikataba mibovu inayoingiwa na watalaamu wa shirika hilo.

Lissu alilaani utaratibu mbovu wa shirika hilo wa kupitisha maji kwenye mabomba na umeme juu ya nguzo, lakini wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wanasikia na kuona faida kwa wengine.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia aliitahadharisha Serikali kuhusu mpango wa kutandaza bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Tanga akisema anaamini hawatakubali kwani wanaona mpango huo hauna faida kwao.

“Watu wa Kusini hawatakuwa tayari kuona mabomba ya gesi yakipita katika mashamba na karibu na nyumba zao wakati wao hawanufaiki na mpango huo,”alisema Ghasia.

Ghasia alisema kitendo hicho kinawakwaza na kuwavunja moyo wananchi wa maeneo hayo jambo litakalochangia kuhujumu miundombinu hiyo.

Akijibu hoja ya Mrema kuhusu Dowans, Waziri Ngeleja alisema,”Mheshimiwa Mrema, ili maisha yaende ni vyema watu wakasahau historia ile. Tuliitana majina mbalimbali, lakini sasa tunasema hivi:

“Serikali haikununua mitambo hiyo, imesema inataka umeme. Ikatokea kampuni ikaiona mitambo hiyo kuwa ni bora na kuiambia Serikali itaizalishia umeme.

"Sasa kwa kuwa sisi tunachotaka ni umeme hatuna sababu ya kuhoji tena mitambo hiyo ya Dowans,”alisema.

Ngeleja, pia alimwomba Waziri Ghasia kuwa mtu wa kwanza kuwashawishi wakazi wa Kusini ili waupokee mradi huo wa kuweka bomba la gesi kwa kuwa mipango ya Serikali inafanywa kwa awamu.

“Mipango hiyo inafanywa kwa awamu. Tunaomba ndugu zetu wa Kusini wakubali bomba lipite ili awamu hii imalizike,”alisema.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo alisema Tanesco inakabiliwana changamoto nyingi ikiwamo tatizo la mgawo wa umeme uliotokana na kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa yanayozalisha umeme.

Alisema bwawa la Mtera litafungwa mwezi Agosti mwishoni kutokana na uhaba huo wa maji, lakini Serikali inajitahidi kuweka mipango ya muda mfupi na mrefu kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo

AFUKUA MAITI YA MUMEWE

Ukistaajabu ya Musa...



Maiti ya Keneth ikifukuliwa ili ivalishwe meno ya bandia aliyokuwa akiyatumia enzi za uhai wake Sunday, June 26, 2011 3:22 AM
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ameifukua maiti ya mumewe toka kaburini kwasababu maiti hiyo ilizikwa huku mumewe akiwa amevalishwa meno ya bandia ambayo yalikuwa si ya kwake.
Phyllis Manis hakutaka mumewe apumzike kaburini huku akiwa amevalishwa meno ya bandia ambayo si ya kwake.

Phylis aliifukua maiti ya mumewe, Keneth iliyokuwa imezikwa kwenye makaburi ya Chattanooga, Tennessee ili aweze kumvalisha meno ya bandia aliyokuwa akivaa kila siku.

Televisheni ya WTVC ya Marekani iliripoti kwamba, wakati Keneth alipokuwa amelazwa hospitali kwenye chumba cha watu mahututi, madaktari waliyachanganya meno yake ya bandia na meno ya bandia ya mtu mwingine hali iliyopelekea Keneth avalishwe meno ya bandia ya mtu mwingine.

Baada ya mazishi ya Keneth ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 76, Phylis aligundua waleti na funguo za mgonjwa aliyekuwa amelazwa chumba kimoja na Keneth zikiwa zimechanganywa na baadhi ya vitu vya Keneth yakiwemo meno ya bandia aliyokuwa akiyavaa Keneth enzi za uhai wake.

"Mume wangu amelala kaburini akiwa na meno ya bandia ya mtu mwingine, siwezi kuruhusu hali hii itokee kwani najua yeye mwenyewe asingependa iwe hivyo", alisema Phylis alipokuwa akihojiwa na televisheni ya WTVC.

Msemaji wa hospitali ya Parkridge Medical Centre ambako tukio hilo lilitokea alisema kwamba hospitali inaomba radhi na imekubali kulipa gharama za kuifukua maiti ya Keneth pamoja na kumnunulia meno mapya mgonjwa ambaye meno yake ya bandia alivalishwa Keneth kimakosa.

"Najua sasa mume wangu atapumzika vizuri na pia familia yetu itaweza kupumzika", alisema Phylis baaada ya maiti ya mumewe kufukuliwa ili kuvalishwa meno ya bandia aliyokuwa akiyavaa enzi za uhai wake.

Jumapili, 26 Juni 2011

OCEAN VIEW YACHEKA, SIMBA BADO YANUNA.

Haruna Moshi katika shikashika za mechi.

JINAMIZI la kutolewa kwenye michuano ya kimataifa bado limeendelea kuiandama Simba baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Vital ‘O’ ya Burundi katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Simba, wawakilishi wa Zanzibar, Zanzibar Ocean View jana walianza vema michuano hiyo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi Etincelles ya Rwanda.

Kwa upande wa mabingwa mara sita wa michuano hiyo Simba, wameingia uwanjani ikiwa ni wiki moja tu ipite tangu wang’olewe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili iliyopita.

Katika mechi hiyo, Simba ilikianza kipindi cha kwanza kwa kuliandama lango la Vital ‘O’ lakini kuanzia dakika ya 35 mambo yalibadilika na wapinzani wao kutoka Burundi ndio waliokuwa wakishambulia na kukosakosa kumfunga mara kadhaa kipa Juma Kaseja.

Mchezo ulibadilika kipindi cha pili ambapo timu zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini bila mafanikio ya kuzifumania nyavu.

Akizungumzia mechi hiyo kocha wa Simba Moses Basena alisema mchezo ulikuwa mzuri hasa ikizingatiwa kuwa wachezaji wake bado wana uchovu lakini anaimani watafanya vizuri mechi zijazo.

Naye kocha wa Vital ‘O’ Mousa Ally alisema ameridhika na matokeo kwa vile Simba ni timu kubwa na wamejitahidi kuibana isishinde.

“Simba ni timu kubwa na ndio maana leo tumecheza sana nyuma tukajitahidi kuibana isishinde lakini tukicheza na timu nyingine mtaona hatutacheza mchezo huu, nimefurahia kabisa matokeo,”alisema.

Nayo Zanzibar Ocean View ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Sabri Ramadhani katika dakika ya pili ya mchezo kwa kuunganisha pasi ya Saidi Rashidi kabla ya kuujaza mpira wavuni.

Kuingia kwa bao hilo kuliamsha safu ya ushambuliaji ya Etinceles ambapo katika dakika ya 23 walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Muhir Clever.

Dakika ya 31 Sabri aliifungia timu yake bao la pili lakini Manirakiza Victorie aliisawazishia timu yake ya Etinceles bao hilo katika dakika ya 40.

Huku ikionekana mechi hiyo itaisha kwa sare, Selemani Haji aliipatia Zanzibar Ocean View bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 85 na kuifanya timu yake iongoze kundi A ikiwa na pointi tatu ikifuatiwa na Simba na Vital ‘O’ zenye pointi moja kila moja na Etinceles ikiwa haina pointi mkiani

POLISI RUVUMA WAIBUA MTANDAO WA WASAFIRISHAJI BINADAMU.

MKONO mrefu wa Jeshi la Polisi nchini, umewanasa watuhumiwa wawili wa biashara ya kusafirisha binadamu nje ya mipaka ya nchi.

Watuhumiwa hao ni wakazi wa Bombambili katika Manispaa ya Songea mjini hapa. Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi Makambi ya mjini hapa.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika na biashara ya kusafirisha watu, wakiwamo wanafunzi wa kike kwenda katika nchi jirani, ikiwamo ya Msumbiji.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Michael Kamuhanda ambaye amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Nolasco Mgalula (31) ambaye ni Mwalimu na Suzana Onesmo. Polisi wanasema kwamba waliwakamata watuhumiwa hao Juni 22 mwaka huu.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi liliwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mtandao huo kutoka kwa raia wema.

Aidha wazazi wa wasichana hao walikumbwa na wasiwasi baada ya kutowaona mabinti zao ndipo walipotoa taarifa za kupotelewa katika Kituo cha Polisi cha Songea mjini.

Kamanda Kamuhanda aliwataja kwa majina wasichana waliotoroshwa (majina tunayahifadhi) na kusema walipelekwa Msumbiji kwa lengo la kufanya biashara za kuuza baa na wengine kufanya kazi ya ukahaba katika madangulo maalumu.

Watoto waliotolewa taarifa wamebainika kuwa ni wanafunzi wa kidato cha pili katika shule za sekondari zilizopo mjini hapa.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha Polisi wamesema kwamba jitihada za kuwapata mabinti hao na kuwarudisha hapa nchini zinafanyika kwa kushirikiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Niasa nchini Msumbiji.

Alifafanua kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kuufuatilia mtandao huo kwa ukaribu zaidi ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinapingana na haki za binadamu na sheria ya elimu nchini kwa kuwa waliofanyiwa kitendo hicho ni wanafunzi.

Alitoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto wanaosoma mkoani hapa kuwa waangalifu kwa mabinti zao kujihusisha na watu waovu hasa wakati huu ambao mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani ya Msumbiji umekuwa mkubwa baada ya kujengwa kwa Daraja la Mkenda katika Kata ya Mitomoni, Songea Vijijini linaloziunganisha nchi za Tanzania na Msumbiji

LOWASA AISHAURI SERIKALI


Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akichangia bungeni, makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
ASEMA INAOGOPA KUFANYA MAAMUZI MAZITO
Kizitto Noya, Dodoma
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa ameiambia Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa inasumbuliwa na ugonjwa wa woga katika kutoa uamuzi magumu na matokeo yake mambo yake mengi hayaendi kama yalivyopangwa.Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika utawala huu wa awamu ya nne, pia akaitaka Serikali hiyo kubadilika.

Alisema kuwa ni bora kulaumiwa kwa kufanya uamuzi mgumu kuliko kulaumiwa kwa kutofanya uamuzi na kwamba Serikali inapaswa kufanya maamuzi bila kujali matokeo yake huku akipendekeza kwa kuanzia, ikope kwa kutumia rasilmali za nchi.

Alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012.
"Ni bora kulaumiwa kwa kufanya maamuzi kuliko kulaumiwa kwa kutofanya maamuzi kabisa,"alisema Lowassa.

Bila kueleza ni maamuzi gani ambayo serikali hiyo imeshindwa kufanya, Lowassa alisema ugonjwa wa viongozi kuogopa kufanya maamuzi ni hatari kwa uchumi wa taifa kwa kuwa kuthubutu ni msingi wa mafanikio katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

"Kuna ugonjwa wa kutokutoa maamuzi hapa na lazima tukubali kubadilike. Ni heri mtu ukosee kutoa maamuzi kuliko kukaa kimya kabisa, heri uhukumiwe kwa kutoa maamuzi kuliko ulaumiwe kwa kushindwa kutoa maamuzi,"alisema.

Lowassa alitoa kauli hiyo huku serikali ikionekana kushindwa kutatua matatizo mbalimbali yaliyoko nchini hivi sasa ikiwemo matatizo ya usafiri wa reli, msongamano na makontena bandarini na ujenzi wa bandari pamoja na taifa kukabiliwa na mgawo wa mara kwa mara wa nishati ya umeme uliodumu tangu mwaka 2006.

Kabla ya Lowassa hajasisitiza suala la kutoa maamuzi, alitumia muda mwingi kuishauri Serikali itenganishe Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kueleza mafanikio ya chama tawala, CCM na Serikali katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuwa ni kubwa mno, hivyo inastahili kugawanywa kwa kuiondoa ofisi hiyo ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

"Ofisi hii ni kubwa sana, kuna Maafa, Uratibu, Bunge, Uwezeshaji, Uwekezaji na Tamisemi. Tamisemi yenyewe pia imegawanyika katika mambo mengi sana.

Nashauri Serikali itafakari kuigawa Ofisi ya Waziri Mkuu ili Tamisemi iwe yenye kujitegemea. Kwa kuwa sehemu katika Ofisi ya Waziri Mkuu inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, haina budi kupunguziwa mzigo,"alisema.

Mbunge huyo alizidi kueleza, "Muundo huu wa sasa haufai. Tamisemi iwe inayojitegemea ili ifanye kazi zake vizuri zaidi kwani Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa mno na ina majukumu mengi." Kuhusu mafanikio ya CCM na Serikali, Lowassa alisema, sio vyema kubeza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha miaka 50 baada ya uhuru au kuyatenganisha na mafanikio ya CCM.

"Miaka 50 ya Uhuru ni historia ya CCM na serikali yake, uongozi wake umefanya mengi na siyo vizuri mambo hayo yakabezwa. Watu wanabeza mafanikio hayo, tusiwakubalie. Miaka kumi tu iliyopita CCM imefanya mengi,"alisema Lowassa na kuendelea:


"Mwalimu aliwahi kusema, akija mtu jeuri na fedhuri akakuuliza Tanzania mna nini? Mwambie tuna amani. Tanzania tuna amani na kwa amani hiyo  tumejenga reli ya Tazara(Tanzania na Zambia), Watanzania wanajua na dunia inajua."

Aliendelea, "Kwa amani hiyo tumejenga shule nyingi za msingi na sekondari, Watanzania wanajua na dunia inajua, amani hiyo tumejenga Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho ni kikubwa katika ukanda wote wa Afrika Mashiriki na Kati, Watanzania wanajua na dunia inajua. Unawezeje kuiondoa CCM katika mafanikio hayo makubwa ya nchi yetu?."

Alisema pamoja na mafanikio hayo yote na yale ya uchumi wa nchi kukua kwa asilimia saba, bado nchi ni maskini na kwamba Serikali sasa inapaswa kuhakikisha uchumi huo unaonekana katika maisha ya kawaida ya Watanzania.

Lowassa alisema Serikali inapaswa kufanya maamuzi bila kujali matokeo yake na akapendekeza kwa kuanzia, ikope kwa kutumia rasilmali za nchi ili kujenga reli ya kati na kuboresha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

"Tutumie utajiri wetu wa gesi kukopa ili tujenge reli na bandari, tufanye hili sasa. Kama tulijenga chuo kikuu kikubwa Afrika Mashariki na Kati, Udom, tutashindwaje kufanya hilo ?,"alihoji.

Akizungumzia matatizo ya jimbo lake la Monduli, Lowassa aliishukuru Serikali kwa kuwapelekea chakula wananchi waliokumbwa na njaa mwaka jana na akaiomba tena ifanye hivyo mwaka huu kwa kuwa hali bado siyo nzuri.

"Nakupongeza wewe mheshimiwa spika kwa kuteuliwa kuliongoza bunge, nampongeza mheshimiwa waziri mkuu, mawaziri, manaibu mawaziri, wabunge wote na wapiga kura wangu wa Monduli,"alisema Lowassa alipoanza kuchangia hoja hiyo.

 Aliendelea, "Kwa kuwa wapigakura wangu wamenipa heshima kubwa kwa kunichagua tena kwa zaidi ya asilimia 90, nipende tu kuwaahidi kuwa nitawapa utumishi uliotukuka. Lakini, nasikitika sana kwa tatizo la njaa na kuishukuru Serikali kusaidia kuokoa maisha ya watu hao. Naiomba Serikali ipime tabianchi, ili tuone nini kitatokea tena ili kama ni kuhama, watu hao wahame."

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza bungeni tangu ajiuzulu Uwaziri Mkuu mwaka 2008 kwa sakata la zabuni tata iliyoipa kazi ya kufua umeme wa dharura Kampuni ya Richmond Development (LLC).

Viongozi wengine waliojiuzulu kutokana na kashfa  hiyo ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha

ATANGAZWA AMEFARIKI KUMBE KAZIMIA TU, DU! MADAKTARI MMESOMA LAKINI MMMH...!?

Atangazwa Amefariki, Azinduka Ndani ya Jeneza, Afariki Tena


Mwili wa Fagilyu Mukhametzyanov ukiwa umezungushwa kwenye kapeti baada ya kufariki kweli mara ya pili
Saturday, June 25, 2011 3:51 AMAlizunduka ghafla na kujikuta akiwa ndani ya jeneza watu wakiiaga maiti yake kabla ya kuzikwa, alikumbwa na mshtuko mkubwa baada ya kuambiwa kuwa madaktari walishaitangazia familia yake kuwa amefariki, kwa mshtuko huo alifariki kweli.
Wakati ndugu na jamaa huku wakiombeleza wakipita mbele ya jeneza lake ambalo liliachwa wazi kwa juu, Fagilyu Mukhametzyanov alizinduka na kuanza kupiga kelele baada ya kusikia watu wakisali kuiombea maiti yake iwekwe mahali pema peponi.

Fagilyu Mukhametzyanov mwenye umri wa miaka 49 wa mji wa Kazan nchini Urusi alitangazwa kimakosa na madaktari kuwa ameiaga dunia wakati alipokumbwa na shambulio la moyo nyumbani kwake na baadae kupoteza fahamu kabisa.

Mume wa Fagilyu, Fagili Mukhametzyanov, 51, aliambiwa na madaktari kuwa mkewe ameiaga dunia kutokana na shambulio la moyo.

Taratibu za mazishi zilianza na wakati watu wakiliaga jeneza, Fagilyu alizunduka ghafla na baada ya kugundua yuko ndani ya jeneza alipiga kelele.

Alikumbwa na mshtuko mkubwa uliopelekea apatwe na shambulio la moyo, aliwahishwa hospitali ambapo alilazwa kwenye chumba cha watu mahututi lakini safari hii aliweza kuishi kwa dakika 12 tu ndipo alipoiaga dunia kikweli kweli.

"Nina hasira sana na nataka majibu ya mambo yaliyojitokeza, hakuwa amefariki wakati alipotangazwa amefariki, wangeweza kuyaokoa maisha yake", alisema mumewe kwa hasira.

Msemaji wa hospitali, Minsalih Sahapov alisema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hili

Alhamisi, 23 Juni 2011

MBOWE ARUDISHA GARI LA SERIKALI, SASA SHUGHULI ZAKE ATAFANYAJE?

Mh. Freeman Mbowe


Kizitto Noya, Dodoma na Raymond Kaminyoge, Dar
OFISI ya Bunge imemtaka Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kususia pia huduma zingine anazopewa na Serikali kulingana na wadhifa wake, badala ya kukataa gari, dereva na mafuta pekee.Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema huduma zote anazopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni zipo kisheria, hivyo hawezi kuchagua masharti anayotaka kuyafuata na mengine kuyakataa.

"Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza:
"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."

Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge.

"Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

Juzi baada ya kupitishwa Bajeti ya Serikali, Kambi ya Upinzani ilitangaza mgogoro na Bunge wa kutochukua posho za vikao vya Bunge kuanzia jana. Lakini hili lingefanyika baada ya kuwasilisha taarifa rasmi bungeni jana.
Sakata la kugomea posho za vikao, lilitangazwa kwa mara ya kwanza na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe na tayari ameandika barua ya kuikataa posho hiyo.

Hata hivyo, wakati kambi hiyo ikitoa msimamo huo wa pamoja, Mbowe alitangaza kuacha kutumia gari alililopewa na Serikali, dereva na mafuta kama sehemu ya kuonyesha kutoridhishwa na hatua ya Serikali kudharau mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na kambi hiyo kuiboresha bajeti.

"Tumewaita hapa kueleza msimamo wetu kama Kambi ya Upinzani baada ya Serikali kuyakataa baadhi ya mapendekezo yetu. Serikali haikukubaliani nasi kuondoa sitting allowances (posho ya vikao),"alisema Mbowe na kuongeza:
"Haikukubaliana nasi pia kuuza mashangingi ya anasa, kuondoa misamaha ya kodi kwenye makampuni ya madini, katika susala la pension kwa wastaafu na kupunguza gharama za kuwasafirisha viongozi wa umma kwenye first class (daraja la kwanza)."

"Sisi tunaamini kuwa viongozi wanaopaswa kusafirishwa kwa ndege katika daraja la kwanza ni Rais na mke wake, Makamu wa Rais na mkewe, Waziri Mkuu na mke wake, Spika wa Bunge na mwenza wake. Halafu mawaziri wanapaswa kusafiri kwa daraja la kawaida na wabunge wote,"
Aliendelea" Na kwa kuwa hawataaki kukubaliana nasi kuuza magari ya fahari, mimi kuanzia sasa (juzi), silitaki gari lao, dereva wao na hata mafuta yao, habari ndio hii."

Barua ya Chadema haijafika Ofisi za Bunge
Lakini Joel alisema kuwa hadi jana mchana, hakuwa amepokea barua yoyote kutoka Chadema ya wabunge wake kukataa posho wala Mbowe, kugoma kuendelea kulitumia gari, dereva wala mafuta.

"Siwezi kufanya kazi kwa taarifa za vyombo vya habari. Mbowe hajanipa gari wala sijapata barua ya wabunge kukataa posho. Mambo hayo yapo kisheria muulizeni (Mbowe) kanipa lini gari hilo?"alihoji

Bunge kuendelea kuwalipa posho
Kuhusu wabunge hao kutochukua posho, Joel alisema posho hizo hazitasitishwa kutolewa kwao hadi utaratibu utakapobadilishwa. "Haya mambo yapo kisheria jamani, nisipowalipa posho mimi nashtakiwa," alisema.

Aliendelea"Mbunge anapewa posho kama sharti namba 3. Sasa kusitisha posho hizo ni mlolongo mrefu ambao hauwezi kufanyika kwa haraka kiasi hicho. Kinachoweza kufanyika, ni kila mbunge anayetaka kutochukua posho kuniandikia barua na sio kama kambi kwa sababu posho hizo ni za mbunge."

Akishaniandikia barua, alisema " Kuna njia mbili; moja ni mimi kumpa posho yake halafu yeye airudishe serikalini au mimi niikatie risiti halafu niirudishe serikalini, lakini haiwezi kupelekwa kwingine kokote zaidi ya kuwapa wabunge wenyewe."

Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa?

Lissu adai Mbowe alirejesha shangingi
Mbowe jana hakupatiakana ofisini kwake kuzungumzia suala hilo, lakini, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisisitiza kuwa tayari alirejesha gari hilo tangu Jumatatu.
"Ni kweli barua hatujapeleka ila itapelekwa kesho, lakini tayari Mbowe amerudisha gari hilo tangu juzi (Jumatatu) na ameanza kutumia usafiri binafsi," alisema Lissu.

… apongezwa kwa kurudisha shangingi
Katika hatua nyingine, baadhi ya wanasiasa, wasomi na wananchi wamepongeza uamuzi wa Mbowe wa kurudisha gari la Serikali ili kuipunguzia gharama za uendeshaji.
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliunga mkono uamuzi huo na kusema hata katika nchi tajiri viongozi wenye nyadhifa za uwaziri wanatembelea magari ya kawaida.

“ Uingereza nchi tajiri, lakini mawaziri wake wanatembelea vigari vidogo vinaitwa Austin, lakini sisi na umaskini wetu mawaziri wanatembelea magari ya kifahari,” alisema Mtikila na kuongeza.
“ Inashangaza sisi walalahoi, lakini viongozi wanatembelea magari ya kifahari kuwashinda wanaotupa misaada, hivi viongozi hawa hawajifunzi,” alisema Mtikila.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii.
Dk Bana alisema ingawa hoja hiyo inamjenga Mbowe kisiasa, lakini ukweli unabaki kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kuyahudumia magari hayo.

Naye Shaaban Mtawa, fundi wa magari wa Kinondoni jijini alisema kitendo cha Mbowe kurudisha gari hilo kimemfurahisha na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano huo.
“Viongozi wengi wanaishi Dar es Salaam, wanatembelea magari ya kifahari bila ya sababu ya msingi wakati yanatumia fedha nyingi,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu.

“Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?,” alihoji Mtatiro.
Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida

PICHA YA LEO; SHAABAN DEDE AKIWA SIKINDE ENZI HIZO,VIPI HUKARIBISHI WENZIO?

Shaaban Dede kiongozi wa Sikinde enzi hizo akiwa na Juma Choka na Mnyupe.

KOCHA MPYA CHELSEA

Villas-Boas kuwa kocha mpya wa Chelsea

Andre Villas-Boas atakuwa meneja mpya wa Chelsea, BBC inafahamu.
Andre Villas-Boas
Andre Villas-Boas akisherekea na wachezaji wa FC Porto Ushindi wao

Alijiuzulu kutoka timu ya Porto siku ya Jumanne baada ya kuisaidia kushinda ligi za Ureno na ligi ya Europa msimu uliopita.
Porto imepokea malipo ya pauni za Uingereza milioni £13.3m kiwango ambacho kipo kwenye mkataba wa Villas-Boas,kutoa nafasi kwa yeye kuondoka.
Chelsea, ambayo imemfuta kazi Carlo Ancelotti mwezi Mei, wameeleza nia yao na tayari wanajadiliana masuala ya mkataba na kocha huyo mwenye umri wa miaka 33.

Chelsea kujadili mkataba na Villas-Boas

Roman Abramovich
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich
" Tunatarajia kukubaliana naye juu ya masuala binafsi ya mkataba na kutoa tangazo rasmi baadaye,"taarifa kutoka kwa timu ya Chelsea ilisema.
Katika taarifa kutoka Porto, timu ya Urenoi inasema kuwa nafasi ya Villas-Boas imechukuliwa na naibu wake Vitor Pereira,ambaye alitia saini mkataba wa misimu miwili.
Rais wa Porto Jorge Pinto da Costa amesema kuwa hajashangazwa na kuondoka kwa Villas-Boas na kusema: " ''Alipokwenda kwa mapumziko ya wikiendi London mwezi mmoja uliopita,nilizungumza na Vitor Pereira na nikamuuliza kama atakuwa tayari kuchukua nafasi hio.Akaniambia yuko tayari na hapo nikaridhika.

WACHUNGAJI WA NIGERIA WANA UTAJIRI MKUBWA KAMA WAFANYABIASHARA YA MAFUTA.

Mchungaji Gwajima wa Tanzania

Mchungaji Getrude Rwakatare wa Tanzania
Wahubiri wa Nigeria wamefanikiwa katika miradi yao na kuwa na utajiri unaolinganishwa na matajiri wanaofanya biashara ya mafuta.
Kwa mujibu wa muandishi wa blogu moja huko Nigeria aliyefanya utafiti wa wahubiri hawa wa neno la Mungu ameiambia BBC kuwa wana Biashara kabambe utadhani wana visima vya mafuta.
Waumini wakibarikiwa

Mhubiri afaidi baraka zake

Mfonobong Nsehe, mwandishi wa blogu ya jarida la kibiashara la Forbes anasema kuwa ma- pastor wanamiliki biashara kubwa kuanzia hoteli kubwa hadi biashara za chakula, mfano wa vyakula vya haraka kama vile 'nyama na kuku'' sawa na Kentucky' ambazo ni vivutio kwa familia na vijana.
Mwandishi huyu anasema kuwa"Uhubiri ni biashara kubwa. Faida yake ni sawa na biashara ya mafuta ya petroli.
visima vya mafuta
Kituo cha Mafuta.

Alitoa mfano wa utajiri wa Wahubiri watano ambao wana takriban dola milioni 200m.
Kanisa za wahubiri wa aina hii zimeimarika nchini Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, ambapo maelfu kwa maelfu wameshiriki na kujiunga nazo.
Bw.Nsehe anasema Mhubiri anayeongoza kwa utajiri, Bishop David Oyedepo wa Kanisa lijulikanalo kama Living Faith World Outreach Ministry, alikadiriwa kuwa na utajiri wa takriban dola milioni150.
Bishop Oyedepo anamiliki kampuni ya kuchapisha, Chuo kikuu, shule moja ya msingi ya kifahari, ndege zake nne za binafsi za kifahari na nyumba kadhaa mjini London na Marekani.

Jumanne, 21 Juni 2011

MRISHO NGASSA KUCHEZA NA MANCHESTER UNITED


Ngassa
Calvin Kiwia na Imani Makongoro
BAADA ya kupata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Seattle Sounders ya Marekani, kiungo mshambuliaji wa Azam, Mrisho Ngassa amesema itakuwa kama ndoto katika maisha yake kucheza dhidi ya Manchester United.

Ngassa anayetajwa kuwa mshambuliaji mahiri katika kizazi hiki, anatarajiwa kuondoka nchini Julai 6, kwenda Marekani kwenye ma
Mrisho Ngassa

jaribio ya kucheza soka ya kulipwa na klabu hiyo kuanzia Julai 13 na ataivaa Manchester United inayofundishwa na Sir Alex Ferguson, Julai 20 kwenye Uwanja wa Qwest Field jijini Seattle.

Ngassa aliliambia gazeti hili jana jijini Dar es Salaam kuwa hakuwahi kufikiri hata siku moja katika maisha yake ya soka inaweza tokea kwake kucheza na dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester United na kusema lakini hiyo yote ni mipango ya Mungu.

"Ni historia mpya naweka katika maisha yangu ya soka, vile vile mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza dhidi ya klabu hiyo kubwa dunia," alisema Ngassa.

Alisema ni kama bahati kwake kupata nafasi hiyo kutokana na Tanzania kusheheni wachezaji wengi na wenye vipaji hivyo kuichukulia kama changamoto kwake kuongeza bidii katika mazoezi na kujituma zaidi.

"Sina budi kuongeza juhudi zaidi kwa kujituma katika mazoezi na kujitunza kama mchezaji, nafikiri nikizingatia yote hayo nitafanikiwa katika ndoto zangu nilizojiwekea za kufika mbali kisoka," alisema.

Alisema anaushukuru uongozi wa klabu ya African Lyon kutojali timu anayoichezea na kumpatia nafasi hiyo ya kwenda kufanya majaribio na klabu hiyo ya Marekani.

"Nafikiri uongozi wa African Lyon ni mfano wa kuigwa katika soka la nchi yetu kwa kitendo cha kiungwana walichokifanya kwangu," alisema.

Alisema uongozi huo ungeweza ukampa nafasi hiyo mchezaji wao Adam Kingwande, lakini umekubali uwezo wa Ngassa na kumpatia nafasi hiyo.

Hata hivyo aliwataka Watanzania kumuombea dua ili aweze kufuzu majaribio hayo na kujiunga na timu hiyo kwani atakuwa akiitangaza Tanzania.

Naye Makamu wa Rais wa timu hiyo, Lance Lopes, alisema kumchukua Ngassa ni kuthamini uwezo wake na mchango akiwa kwenye timu mbalimbali, ikiwamo ile ya taifa, Taifa Stars.

Alisema amekuwa akitumia akili nyingi kucheza soka, hivyo kwa kufanyiwa majaribio ya wiki mbili akiwa kwenye timu yao, hadi kwenye mechi ya kirafiki na mabingwa wa England na mabingwa mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester United ni jambo la kuijivunia kwa historia ya soka Tanzania.

"Sisi kama wadau wa michezo hasa mpira wa miguu duniani, tunajisikia raha kumfanyia majaribio mchezaji wa Tanzania, Ngassa huku tukijua fika inaweza kuwa chachu kwake, ukizingatia kwamba Manchester United wataweka kambi kwetu kuanzia Julai 13, ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu ya England.

"Huu ni wakati wake sasa wa kufanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba nafasi hii anaitumia vyema, maana dunia nzima inaweza kumuona na kuthamini kipaji chake, ukizingatia kwamba yeye atakuwa mchezaji wa kwanza kufanya majaribio kwa timu kubwa inayokipiga pia na timu kubwa duniani,” alisema Lopes.

Naye Mwenyekiti wa timu ya Azam FC, Mohamed Said, alisema katika makubaliano hayo ya kumfanyia majaribio Ngassa hawajaangalia sana maslahi ya fedha zaidi ya kumuwekea ramani mchezaji wao.

Alisema endapo Ngassa anatafakiwa kufuzu kwenye timu hiyo, mafanikio yatakuwa kwa Tanzania nzima, huku akiitumia nafasi hiyo kumuasa mchezaji huyo mwenye kasi anapokuwa uwanjani.

Tumekuwa katika shauku kubwa ya kuona Tanzania inafanikiwa kuwa na wachezaji wengi duniani na kuwa na msaada na nchi, hivyo naamini uwezo wake ni mkubwa na unaweza kuwa na tija kwake.

Ni mchezaji mzuri, ndio maana amekuwa na msaada mkubwa kwenye timu mbalimbali, Azam FC, Yanga na hata anapokuwa kwenye timu ya Taifa, Taifa Stars, amekuwa akifanya vitu adimu kutokana na kipaji chake,” alisema.

Ngassa aliwahi kupata nafasi ya kufanya majaribio na klabu ya West ham ya Uingereza iliyokuwa ikinolewa na kocha Gionfranco Zola ambayo imeshuka daraja msimu huu lakini hakufanikiwa kufuzu majaribio hayo.

CHANZO; GAZETI MWANANCHI

MAMA AMWAGIA RADHI MWANAE KUTOKANA NA TABIA YAKE YA UKAHABA.

KATIKA hali ambayo iliwaacha watu wengi wakiwa hawaamini macho yao mwanamke mmoja [51] amejikuta akisaula nguo zake zote na kutoa radhi hadharani kwa mwanae wa kike aliyefahamika kwa jina moja la Feti[22] kwa kile kilichodaiwa kuchoshwa na tabia zake
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya jioni huko maeneo ya Buguruni Mnyamani ambapo imedaiwa mama huyo alichoshwa na vitendo vinavyofanywa na mwanae huyo ambavyo vilikuwa havimridhishi.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, mama huyo jana majira ya jioni aliamua kumtolea uvivu mwanae huyo kwa kusaula viwalo alivyokuwa amevaa akiwa na lengo la kumtolea radhi.

Awali imedaiwa kuwa Feti alikuwa na tabia za kumdhihaki Mungu kwa kufanya matendo maovu yanayodaiwa yanaenda sambamba na ukahaba ambapo mama huyo imedaiwa alikuwa akimpigia kelele kila kukicha mwanae huyo ambaye alikuwa hataki kufuata yale anayoambiwa.

Pia imedaiwa kuwa Feti amekuwa na tabia za kugombana na wake za watu ikiwa ni pamoja na kufumaniwa na waume za watu mara kwa mara katika mtaa anaoishi hali iliyopelekea kuidhalilisha familia yake.

Hata hivyo kutokana na vitendo na tabia chafu za Fet, mama huyo alijitoa kimasomaso kumlaani mwanae huyo jana wakati binti yake huyo alipokuwa katika matayarisho ya kutoka safari zake za usiku.

Ilidaiwa na shuhuda wa tukio hilo kuwa mama huyo alianza hivi” Yaani ukitoka tu hapa ndani kwenda katika biashara zako za kishenzi naomba ugongwe na gari ufe papohapo” hata hivyo imediwa kuwa Fet hakutishika na kauli hizo na alitoka kinguvu na mama huyo alianza kulia kwa uchungu na kuanza kusaula viwalo alivyokuwa amevaa huku akishikwa na baadhi ya majirani zake waliomsihi kuacha kufanya hivyo huku Feti akitimua mbio na kutokomea kusikojulikana.

Hata hivyo imedaiwa kuwa msichana huyo alikwenda kuomba hifadhi nyumba ya jirani kutokana na aibu aliyoipata kutoka kwa mama yake huyo

MASHOGA WARUHUSIWA KUWA MAKASISI UINGEREZA, DUNIA INAELEKEA KUBAYA AU!?

Mashoga Kuwa Mapadri Uingereza


Mchungaji ambaye pia ni shoga, Dr Jeffrey John
Jumuiya makanisa ya Anglikana, Uingereza inatarajiwa kutangaza rasmi kuwa wanaume waliojitangaza wazi kuwa wao ni mashoga wataruhusiwa kuwa mapadri iwapo watatimiza sharti la kujizuia kufanya ngono
Taarifa rasmi ya kuruhusu mashoga kuwa mapadri inatarajiwa kutolewa jumatatu ambapo imetangazwa kuwa ni katika kuondoa ubaguzi katika masuala ya dini bila ya kuwabagua watu kwa tabia au matendo yao kinyume na maumbile.

Sharti la kuwataka mashoga wajizuie kufanya ngono iwapo wanatakiwa kupewa nafasi hiyo kubwa ya kidini huenda ikasababisha mtafaruku kwani mchungaji mmoja shoga anapinga sharti hilo na anatishia kujitoa yeye na wafuasi wake duniani toka kwenye kanisa hilo.

Mwaka 2003, mchungaji ambaye pia ni shoga na mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Dr Jeffrey John alitajwa jina lake miongoni mwa wagombea wa uaskofu wa mji wa Reading hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa kwenye kanisa la Anglikana na kupelekea aamue kulitoa jina lake.

Kanisa la Anglikana halitaki mgogoro wowote utokee na kuwagawa waumini wa kanisa hilo duniani.

Hata hivyo, baadhi wa waumini wa kanisa hilo la Anglikana wanapinga uamuzi wa kuruhusu mashoga kuwa mapadri kwani ni kinyume na mafundisho ya kanisa

HIVI HIZI ATM ZINAFANYA KAZI MASAA 24 KWA SIKU KAMA WANAVYOSEMA AU!? INASEMEKANA KILA JIONI HUWA ZINAZIMA MASAA KADHAA, KWELI?

NMB Nachingwea mida ya jioni mambo ni yaleyaleeee.....

Hawa nao kabla muhamala haujakamilika walitoka nje mara kadhaa, mimi nilitaka kamili nikapata nusu ya nilichokiomba, tutafika tu msijali!

Jumamosi, 18 Juni 2011

KIOTA KINGINE CHA MARAHA CHAIBUKA NANGURUKURU, MISOSI KIBAO,NI KAMA KILE CHA KITONGA COMFORT

A Starcom Nangurukuru Lodge, kitu kimetulia maana tulikuwa tunakosa hata sehemu ya kujihifadhi tukiwa safarini, salaam kwa marketing assistant Anil wa Kigogo.

KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA, NGYUEN AOMBA MSAADA WA MATIBABU

PICHA - Kabla Hujafa Hujaumbika....




Nguyen Duy Hai akiwa amezungukwa na watu walioenda kumtembelea Saturday, June 18, 2011 7:58 AM
Wahenga hawakukosea waliponena kuwa kabla hujafa hujaumbika, mwanaume huyu wa nchini Vietnam, anaomba msaada toka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa operesheni ya kuuondoa uvimbe kwenye mguu wake wenye uzito wa kilo 80 na urefu wa mita moja.
Kijana Nguyen Duy Hai wa nchini Vietnam, hawezi kufanya kitu chochote zaidi ya kukaa chini au kujilaza kwani uvimbe kwenye mguu wake umekuwa mzito sana kiasi cha kufikia uzito wa kilo 80 hivyo kuunyanyua mguu wake ni sawa na kuzinyanyua kilo 80 toka chini.

Uvimbe huo ambao hautokani na kansa uliopo kwenye mguu wake wa kulia, unachukua nafasi yenye urefu wa mita moja kiasi cha kuingia kwenye rekodi ya uvimbe mkubwa kuliko yote iliyowahi kurekodiwa nchini Vietnam.

Uvimbe kwenye mguu wa Nguyen ulianza alipokuwa na umri wa miaka 14, ambapo ulipozidi kuwa mkubwa ulipelekea kukatwa kwa mguu wake lakini umeendelea kukua kila miaka ilivyoenda na hivi sasa Nguyen akiwa na umri wa miaka 31 hawezi tena kufanya chochote zaidi ya kulala au kukaa.

Umaskini wa familia yake ndio sababu ya Nguyen kushindwa kwenda hospitali kufanyiwa operesheni ya kuondolewa uvimbe huo.

Kilio chake cha kuomba msaada toka kwa wasamaria wema duniani kimepelekea habari kuhusiana na uvimbe wake kusambaa haraka kwenye vyombo vya habari duniani.

Nguyen anatumaini kuna mtu atajitokeza kulipia gharama za matibabu yake hivyo kumuondolea mzigo mama yake mwenye umri wa miaka 61 ambaye hivi sasa ndiye anayemuuguza wakati wote.

Gonga linki chini kuangalia picha za Nguyen.

Alhamisi, 16 Juni 2011

MITAA YA NACHINGWEA LEO, UNACHEKI NGUNJA HIYO!? NYUMBA ZA MITI NA UDONGO KUMBE NI IMARA SANA.

Mitaa ya Majengo J,vumbi jekundu la kumwaga, nyumba imara za miti na udongo.

Bustani ya kunde nje kama kawaida

Kanisa kuu la katoliki Nachingwea

Soko la baiskeli ni kubwa sana.
Wastani kila nyumba ina baiskeli moja kwa vile maji ni shida hivyo ni muhimu kwa kubebea maji.

PICHA YA LEO;AJITUNDIKA NDOANO KUPINGA KUVULIWA SAMAKI AINA YA PAPA HUKO UINGEREZA.

BAJETI YA UPINZANI YASIFIWA.

Waziri kivuli wa fedha Zitto Kabwe.

Upinzani Bungeni, imesomwa jana na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Bw. Kabwe Zitto na kuonekana kuwa na tofauati kubwa na ile iiyowasilishwa na Waziri Mustapha Mkulo
Hotuba hiyo ilitoa mapendekezo mfumo mzima wa kulipana posho za vikao uondoke katika utumishi wa umma na ziruhusiwe posho za kujikimu kama viongozi au watumishi wakiwemo na maafisa wa umma wanaposafiri nje ya vituo vyao vya kazi.

Kupinga posho za vikao zifutwe mara moja kwa kuwa hazina msingi wowote ni kuiongezea mzigo serikali.

Akifafanua kuhusu posho hizo “ Sisi tulipwe posho za vikao ikiwa ni sehemu la jukumu, mbona polisi halipwi posho kwa kulinda, mwalimu halipwi posho kwa kuingia darasani na mbona nesi halipwi posho kwa kusafisha vidonda vya wagonjwa? Hiisi sahihi zifutwe mara moja? Alisema Kabwe...

Imependekeza kubana kampuni kubwa kulipa kodi inavyostahili, imetoa maoni ya kufutwa kabisa kwa msamaha wa kodi kwenye mafuta kwa kampuni za madini na zile za ujenzi, kwani unasababisha upotevu mkubwa fedha za umma.

Pia imependekeza elimu ya bure kwa Watanzania kuondoa ada za shule za sekondari na kupiga mnada magari ya anasa ya serikali yalipo sasa.

Hotuba hiyo imesema kulifufua Shirika la Ndege (ATCL), ambapo Mashirika ya Umma mengine kama Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) na TANAPA.

Kuboresha sekta nzima ya madini na kufafanua ikisimamiwa vizuri ipasavyo pato linaongezeka kampuni za madini zingewekeza kwenye migodi serilkali itapata faida a fedha kutoka huko kwani mauzo ya dhahabu huishia kulipia madeni na riba hivyo kukosesha serikali mapato

WANAFUNZI UDOM WASIMAMISHWA.

Jengo la Utawala Chuo Kikuu cha Dodoma

CHUO KIKUU cha Dodoma (UDOM) kimefungwa kufuatia kukithiri kwa vurugu zilizokuwa zikizifanywa na wanafunzi chuoni hapo.
Jana Uongozi wa chuo hicho kiliamuru wanafunzi kuondoka eneo la hilo kwa kuwapa masaa mawili wasionekanemaeneo ya chuo na kukitangaza kukifunga kwa kipindi kisichojulikana kuanzia jana.

Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Idris Kikula, alisema jana kuwa, uamuzi wa kukifunga chuo hicho una lengo la kuepusha baadhi ya wanafunzi na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na baadhi yao kukaidi amri ya kusimamisha mgomo wao uliodumu kwa muda mrefu chuoni hapo.

Kikula amesema uamuzi huo umekuja baada ya wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Sayansi ya Jamii kuilazimisha Serikali kuwapa posho za mazoezi kwa vitendo kabala ya muda.

Amefafanua kuwa, wanafunzi hao wanatakiwa waende kwenye mafunzo kwa vitendo katikati ya mwezi ujao na walishakubalina kuwapa posho hizo lakinis wanafunzi hao wametishia mgomo kuilazimisha Serikali kuwapa posho hizo kwa sasa.

Mgomo huo umesababisha wanafunzi wapatao 400 kusimamishwa masomo na kufuatia hali hiyo Profesa Kikula amesema watachapisha majina ya watakaotakiwa kurudi chuoni katika tovuti ya chuo

DROGBA APATA JIKO,BAADA YA MUDA MREFU KULA MAGENGENI.

Hatimaye Drogba Aoa


Drogba na mkewe Lalla Diakite
Baada ya kuishi na mpenzi wake kwa muda mrefu, nyota wa soka wa Chelsea na Ivory Coast, Didier Drogba amefunga pingu ya maisha na mpenzi wake katika harusi ya kukata na shoka ambayo masupastaa wa R&B, wacheza soka na nyota wa NBA walihudhuria.
Mfumania nyavu wa Chelsea, Didier Drogba ameamua kumuoa mpenzi wake wa muda mrefu ambaye amezaa naye watoto watatu kwa kufunga ndoa ambayo sherehe yake ilihudhuriwa na masupastaa mbalimbali.

Drogba mwenye umri wa miaka 33, alifunga ndoa na mama watoto wake, Lalla Diakite mjini Monaco, Ufaransa.

Mmiliki wa Chelsea, bilionea Roman Abramovich ndiye aliyeiongoza harusi hiyo huku Salomon Kalou na Florent Malouda wakiwa wapambe wa bwana harusi.

Nyota wa RnB, Akon na masupastaa wa mpira wa kikapu wa NBA walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika harusi hiyo.

Fally Ipupa toka Jamhuri ya Kongo naye alikuwepo kwenye harusi hiyo sambamba na nyota wa muziki wa Nigeria, J Martins ambaye alipewa usafiri wa bure na Drogba ili aweze kupafomu na Ipupa wimbo wake wa Jupa Remix.

Michael Essien naye alitia maguu kwenye harusi hiyo baada ya kupanda pipa toka Nigeria ambako alishiriki mechi maalumu pamoja na mastaa mbalimbali wa soka duniani kumuaga rasmi Nwako Kanu ambaye amestaafu soka rasmi baada ya miaka 16 ya kulisakaka kabumbu kimataifa.

Jumanne, 14 Juni 2011

MMOJA AUAWA KATIKA UPORAJI MUHIMBILI JANA.



Sabina Masawe aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa kushoto na majambazi Muhimbili akiwa wodini kwa matibabu Tuesday, June 14, 2011 12:08 PM
TUKIO la uporaji fedha lililotokea jana mapema katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umesababisha upotevu wa shilingi milioni kumi na mbili na laki saba ambazo ziliporwa na majambazi waliovamia hospitalini hapo
Tathimini hiyo imetolewa jana na Afisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Bw.Eminael Eligaesha

Eligaesha amesema kuwa, katika tukio hilo jumla ya shilingi million kumi na mbili na laki saba ndizo ziliibiwa katika tukio hilo kwa wahasibu wa hospitalini hapo”CashCollecter” walivamiwa na majambazi hayo na kuporwa mkoba uliokuwa na fedha hizo

Alisema wakusanyaji fedha hao walikuwa wakitumia gari aina ya Pickup walikuwa wakikusanya fedha katika vitengo hospitlaini hapo na walipokuwa wakitoka jengo la OPD kwenda jengo la Uhasibu ghafla walivamiwa na kuzingirwa na watu wapatao sita na walimpiga risasi askari aliyekuwa na watumshi hao na mwingine alijeruhiwa wakati akishuka katika gari hilo na hawakuweza kujitetea na walinyanganywa fedha hizo

Alisema askari huyo alifariki dunia majira ya saa 3 usiku jana katika hospitali hiyo na Bi. Sabina Masawe alijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika paja la kushoto na anaendelea na matibabu hospitalini hapo kubaini kama risasi ipo mwilini ama ilitoka

PICHA YA LEO; HILLARY CLINTON NA JK WAKIAGANA IKULU YA DAR ES SALAAM JANA, WANAMEREMETA.

Mh, Jakaya Mrisho Kikwete na Hillary Clinton jana.

MAHAKAMA YAAMURU ASKOFU AKAMATWE

Askofu Valentino MOKIWA
Mussa Juma, Arusha
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa na Askofu mpya wa Kanisa hilo aliyewekwa wakfu juzi, Stanley Hotay.Askofu Mokiwa, alimweka wakfu Hotay Jumapili, siku mbili tangu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa maagizo ya kusitishwa kwa shughuli hiyo.

Kitendo hicho cha Askofu Mokiwa kuendelea na mchakato wa kumweka wakfu Askofu Hotay pamoja na amri ya Mahakama kutaka shughuli hiyo isitishwe, kimeelezwa kuwa ni dharau kwa mahakama.

Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu huyo zilifanyika juzi Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Claudio Bitegeko na maofisa kadhaa kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Uamuzi wa kukamatwa kwa maaskofu hao, ulitolewa jana na Jaji Kakusulo Sambo baada ya wakili wa mashtaka, Meinrad D’souza kuwasilisha maombi maalumu ya kutaka Mahakama Kuu itoe adhabu kwa Dk Mokiwa na Hotay kwa kukaidi amri ya Mahakama.

Akitoa uamuzi ambao ulichukua takriban saa moja, Jaji Sambo alisema haihitaji elimu ya chuo kikuu chochote kuona kuwa walichokifanya Maaskofu hao wa Anglikana ni dharau kwa amri halali ya Mahakama.

Alisema kitendo walichokifanya ni kudharau Mahakama tena Mahakama Kuu na kwamba kama hatua kali zisipochukuliwa, nchi haitatawalika katika misingi ya sheria.

“Nchi hii inaongozwa kwa misingi ya sheria  na Rais Jakaya Kikwete amekuwa akieleza kuwa kila mtu anapaswa kuheshimu utawala wa sheria. Inasikitisha kama viongozi wa dini wanakiuka sheria, tukiendelea hivi itakuwa tabu sana,” alisema Jaji Sambo.

Alisema mtu yeyote anayeishi Tanzania ni lazima atii na kuheshimu sheria zilizopo hata kama ni raia wa nchi nyingine.Jaji Sambo alisema wasomi wa sheria wanatambua kuwa, Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kifungu cha 37(2) kinaeleza namna ya kuwashughulikia watu wanaokiuka amri ya Mahakama.

Alisema Askofu Mokiwa ameeleza katika tamko lililowasilishwa Mahakamani jana kuwa alimweka wakfu Askofu Hotay kama Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, lakini hatua hii imekuja kabla ya Mahakama haijatoa uamuzi kwa shauri lililokuwa limefikishwa Mahakamani.

“Hii ni sawa sawa na mwenendo mzima wa kesi unakuwa hauna maana tena, kwani tayari Askofu anayelalamikiwa ameapishwa na taratibu za kumpata Askofu ni zilezile ambazo zimelalamikiwa, hivyo kutokana na hali hii, nimeridhika kuwa amri halali imekiukwa,” alisema Jaji Sambo.

Jaji Sambo alisema katika mazingira hayo, ni wazi kuwa kuna namna ya kuwashughulikia wanaokiuka amri halali ya Mahakama.

Alisema Sura 11 ya Kanuni ya Adhabu Cap 16 ya mwaka 2002, inaeleza kuwa ni makosa kuingilia chombo cha utoaji haki na imeeleza ni nini kinaweza kufanyika kwa atakayekiuka.

Jaji huyo alisema Kifungu cha 114 (i) C na K cha CPA, kinafafanua kosa la kuingilia mwenendo wa kesi Mahakamani na katika kifungu hichohicho, kipengele cha tatu kinaipa Mahakama mamlaka ya kumwadhibu mtu anayevunja sheria hiyo.

"Mtu yeyote ambaye anasababisha kuingiliwa kesi au kuvuruga mwenendo wa kesi yupo hatiani,” alisema Jaji Sambo na kuongeza kuwa kifungu cha 124 CPA kinafafanua kuwa mtu anayevunja maagizo ya Mahakama achukuliwe hatua.“Kwa mazingira haya uamuzi mdogo ambao ulipaswa kutolewa leo sitautoa hadi hapo nitakapopanga tena na wahusika watajulishwa.”

"Hivyo katika uamuzi huu wa sasa, naagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Valentine Mokiwa na mlalamikiwa wa pili, Stanley Hotay na taratibu za kujibu kosa hilo la jinai zianze."

Awali, Wakili D’souza alisema kitendo cha Askofu Mokiwa kumweka wakfu Hotay kimeingilia uhuru wa Mahakama na kimeshusha heshima ya Mahakama Kuu, kwani ilitoa agizo la kusitishwa shughuli zozote za kuapishwa kwa kiongozi hiyo.

Hata hivyo, Mawakili wa Utetezi, Joseph Thadayo na Issa Mavura waliomba Mahakama kutokubali maombi ya kuchukuliwa hatua Askofu Mokiwa na Askofu Hotay kwa maelezo kuwa hawakuingilia mwenendo wa kesi hiyo.

Thadayo alimkabidhi Jaji Sambo tamko la Askofu Mokiwa ambalo linaeleza kilichotokea kuwa Hotay amesimikwa kama Askofu wa Anglikana Tanzania na siyo Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.Mara baada ya uamuzi huo, Wakili Thadayo alisema hawana la kufanya zaidi ya kutekeleza maagizo hayo.

“Tutashauriana cha kufanya lakini kwa sasa ndiyo hivyo imeamriwa,” alisema Thadayo

Jumatatu, 13 Juni 2011

UJERUMANI YAWAUNGA MKONO WAASI WA LIBYA.

Ujerumani yawatambua waasi wa Libya

Ujerumani imetambua waasi wa Libya kama "Wawakilishi halali wa wananchi wa Libya".

"Tunataka Libya huru, ya amani na demokrasia bila ya kuwepo Muammar Gaddafi," Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema katika ngome ya waasi mjini Benghazi.

Takriban mataifa kumi na mbili yametambua Baraza la mpito la Taifa.

Ujerumani ilishutumiwa kwa kukataa kuunga mkono azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, la kuruhusu majeshi ya Nato kulinda raia wa Libya.

Baraza hilo la mpito liliundwa na majeshi yaliyoanzisha upinzani dhidi ya utawala wa Kanali Gaddafi, Februari 16.

Baada ya miezi ya mapigano makali, Kanali Gaddafi amesalia na udhibiti wa mji mkuu Tripoli, huku waasi wakishikilia mji wa Benghazi na eneo kubwa la mashariki.

Akizungumza kwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa waasi, Ali Issawi, Bw Westerwelle amesema: "Tuna lengo moja: Libya bila Gaddafi.

"Baraza la taifa ndio wawakilishi halali wa watu wa Libya."

Wananchi wa Libya waliokuwa wakisikiliza, walipiga kofi baada ya tangazo hilo.

Afisa wa ngazi ya juu, makamu mwenyekiti wa baraza, Abdel Hafez Ghoga, amefurahishwa na uamuzi huo wa Ujerumani akisema ni "Hatua kubwa sana".

Wanasdiasa wa upinzani, wanahabari na wataalam wa sera za nje wa Ujerumani, walishutumu serikali kwa kutojiunga na mashambulizi ya Nato, na kuituhumu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kimataifa.

MAJAMBAZI YAVAMIA HOSPITALI YA MUHIMBILI NA KUPORA FEDHA.


Kundi la majambazi wasiofahamika idadi yao wamevamia sehemu ya mapokezi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanikiwa kupora fuko la fedha ambapo haijafahamika mara moja kulikuwa na kiasi gani cha fedha
Uvamizi huo ulitokea asubuhi ya leo na kufanikiwa kumjeruhi askari na mtu mmoja aliyekuwa akihusika na ukusanyaji wa fedha katika vitengo hivyo

Imedaiwa leo wakusanyaji mapato hospitalini hapo walianza kukusanya mapato ya hospitalini hapo na ghafla walipofika eneo hilo walivamiwa na majambazi hayo na kufanikiwa kupora fedha

Jumapili, 12 Juni 2011

MRADI WA MAJI NACHINGWEA UMEFIKIA HATUA NZURI,HONGERA CHIKAWE NA HALMASHAURI YAKO.



Shida ya maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa wilaya ya Nachingwea kwa muda mrefu inaelekea kwisha baada ya juhudi za mbunge na wadau wengine kuzaa matunda kwani mradi wa utandazaji mabomba unaendelea vema.

MICHUANO YA CAF AFRIKA; SIMBA SC YAICHAPA MOTEMA PEMBE BAO 1-0

Shirikisho linaloongoza mchezo wa mpira wa miguu CAF linasema kuwa Libya bado ndiyo iliyopangiwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013.
Hata hivyo Caf linasema kuwa mipango mbadala ipo ikiwa Libya itashindwa kutokana na ghasia za sasa hivi nchini humo.
Waasi wanaotaka kumpindua Kanali Mummar Gaddafi wanadhibiti sehemu kubwa ya mashariki ya nchi hiyo.
Katibu mkuu wa CAF Hicham El Amrani ameiambia BBC kuwa mashindano yote ambayo Libya ilikubali kuandaa siyo tu Kombe la Mataifa ya Afrika bali hata mashindano ya wachezaji wanaocheza soka katika vilabu vya nyumbani CHAN na Futsal bado tunaonelea kuwa ni jukumu la Libya.
Libya iliahidi kuandaa
Mipango mingine ipo

Katika kinyanganyioro cha vilabu klabu ya JS Kabylie imekuwa ya kwanza kufuzu kwa hatua za makundi katika Kombe la shirikisho kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya ASC Jaraaf ya Senegal mechi iliyochezwa ijumaa mjini Tizi Ouzou.
J.S KABYLIE
Mshambuliaji wa Kabylie

Mabao ya Kabylie yalitiwa kimyani na beki Chemseddine Nessakh na kiungo Saad Tedjar kutimiza jumla ya mabao 3-1 kwa klabu hiyo ya Algeria.
Ikumbukwe kuwa klabu hiyo JS Kabylie ilikuwa bingwa wa Afrika mwaka 1981 na 1990.
Wakati huo huo Kufuatia ushindi wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wa 4-0 dhidi ya Primeiro Agosto ya Angola katika mchuano wa kwanza na kutoka sare ya 1 1 katika mecghi ya marudiano nchini Angola, Asec Mimosa inapiga hatua kwa ushindi wa jumla ya bao 5-1 il hali Primeiro itabidi isubiri msimu ujao.
Wakati Primeiro ya Angola ikisubiri fursa ya kushiriki michuano ya Afrika mwakani, watani wao Inter Clube ilisababisha sare ya 2-2 ugenini Morocco dhidi ya klabu ya nchini humo Difaa al Jadida, mechi ya kwanza mjini Luanda ilimalizika kwa Difaa kudundwa matatu kwa bwerere.
Entente Setif ya Algeria ilikuwa nchini Nigeria kuchuana na Kaduna united baada ya ushindi wa 1-0 nchini Algeria tunasubiri matokeo ya mchuano wa mjini Kaduna leo.
mgogoro nchioni Libya
CAF inatafakari mwenyeji mwingine

Na mgogoro wa Libya umeanza kuathiri ratiba ambapo mechi kati ya Sunshine stars ya NIGERIA na Al Ittihad ya Libya ilibadilishwa ifanyike kwa mkondo mmoja badala yua miwili ikitazamiwa kuchezwa kati ya tareh 10 na 12 juni yaani leo
Huko Fez nchini Morocco,l Zesco united ya Zambia ilikuwa uwanjani kwa matumaini ya kuongezea ushindi wao wa bao moja kwa sufuri majuma mawili mjini Lusaka lakini waligutushwa kwa bao mbili za Maghreb Fez na hivyo Fez inapiga hatua kwa ushindi wa 2-1.
Mjini Dar es Salaam Tanzania Simba ya Dar es Salaam illipokea klabu ijulikanayo kama Darling Club Motema Pembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Simba Sports au mnyama kama wapenzi wake wanavyopenda kumuita alimtafuna Motema Pembe 1-0 bao lililotiwa kimiani na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi.
Licha ya ushindi huo Simba ina kibarua itakapochuana na Motema Pembe katika mechi ya marudiano mjini Kinshasa jumapili ijayo. Ina maana Simba haitoweza kupumzika.
Kwa upande mwingine mjini Nairobi Sofapaka iliwapa matumaini mashabiki wake licha ya kuingia uwanjani ikiwa na deni la bao 3-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Club Africain majuma mawili yaliyopita.
Sofapaka ilitumia vizuri uwanja wa nyumbani na kuisukuma Club Africain na kupata magoli matatu ingawa Africain iliweza kufunga bao moja la ugenini.
Bao hilo la ugenini la Africain ndiyo lililoiondoa Sofapaka na kuhitimisha safari yake.