Ijumaa, 27 Januari 2012

BERTRAND TRAORE AMBAYE NI KINDA WA CHELSEA KUCHEZA NA WAKONGWE FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA HURU YA AFRIKA.

Chelsea youngster Bertrand Traore is making his way over to Africa after being named in Burkina Faso's Africa Cup of Nations squad.
The midfielder won his first cap for his country in a friendly match in September and links up at the tournament in Equatorial Guinea and Gabon with older brother Alain, who plays for AJ Auxerre.
Chance: Bertrand Traore will be hoping for a chance to play at the Africa Cup of Nations
Chance: Bertrand Traore will be hoping for a chance to play at the Africa Cup of Nations
If Traore appears in his country's first match, against Angola on January 22, he will be the third youngest player ever to appear in the tournament, at 16 years, four months and 16 days old.
Traore could then find himself facing off against Chelsea team-mates Didier Drogba and Salomon Kalou, who play for the Ivory Coast and complete the group, along with Sudan.
Ghana's Shiva Star Nzigou holds the record for youngest player at 16 years, two months and 30 days old, even scoring during the match against South Africa at the 2000 finals.
Sierra Leone's Mohamed Kallon is second, appearing in the 1996 finals at 16 years, three months and nine days old.
Burkina Faso only confirmed their participation in the cup on Tuesday, when the Court of Arbitration for Sport rejected a case brought by Namibia regarding the eligibility of Burkina defender Herve Zengue.
Zengue was not included in Burkina Faso's 23-man squad for the tournament.

AFRICA CUP OF NATIONS- IVORY COAST YAIFUNGA BURKINA FASO 2-0.

Ivory Coast secured a place in the African Cup of Nations quarter-finals after beating Burkina Faso 2-0 on Thursday.
Salomon Kalou opened the scoring in the 16th minute and Bakary Kone headed in an own goal in the 82nd to hand victory to the pre-tournament favourites despite another unconvincing performance from its English Premier League-based stars.
Party time: Ivory Coast celebrate Salomon Kalou's strike
Party time: Ivory Coast celebrate Salomon Kalou's strike
Earlier, Sudan twice rallied from defensive errors to draw 2-2 with Angola in the other Group B match at Nuevo Estadio de Malabo.
The results mean Angola and Sudan retained hopes of progressing, but Burkina Faso was eliminated with a match to go.
'It was an incredible injustice that we lost this match,' said Burkina Faso coach Paulo Duarte, who refused to talk about his future. 'Burkina Faso played a great match, had a great attitude, but they scored two goals. Football is like that. What more can I say?'
Close marking: Ivory Coast midfielder Yaya Toure is held by Mahamadou Kere
Close marking: Ivory Coast midfielder Yaya Toure is held by Mahamadou Kere
Didier Zokora returned to the Ivory Coast starting lineup after serving a suspension and was the only change from the 1-0 win against Sudan, with Igor Lolo dropping to the bench.
Duarte made three alterations to the team that lost 2-1 against Angola, including forward Prejuce Nakoulma to provide more support for Moumouni Dagano in attack.
Ivory Coast took the lead when Kalou pounced on a low cross that brushed off Yaya Toure, and hit a left-foot shot past Daouda Diakite in the Burkina Faso goal.

BAADA YA KUHUSISHWA NA MASHTAKA NA ICC, UHURU KENYATTA AJIUZULU UWAZIRI.

Kenyatta aachia ngazi

Uhuru
Uhuru anakabiliwa na mashtaka kutoka ICC
Waziri wa fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameachia nafasi yake kufuatia uamuzi kuwa atashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadam.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mahakama ya Kimataifa (ICC) kusema ajibu mashtaka kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008.
Lakini atasalia kuwa naibu waziri mkuu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Mwai Kibaki.
Afisa mwingine wa ngazi ya juu serikalini, Francis Muthaura, pia amejiondoa madarakani.
Wawili hao ni miongoni mwa watu wanne waliotajwa na ICC, ambao wote wanakanusha kuhusika kwao katika ghasia za uchaguzi mwaka 2007-08.
Mwanasheria mkuu wa Kenya alisema sio lazima kwa viongozi hao kujiuzulu, akisema hatma yao ingejulikana baada ya matokeo ya rufaa yao kupatikana ya kuzuia kesi ya Mahakama ya Kimataifa kuendelea.
Bw Kenyatta, ambaye ni mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta, na ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wananchi tajiri zaidi nchini humo, anatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadam, ikiwemo mauaji na utesaji. Bw Muthaura anakabiliwa na mashtaka kama hayo pia.
Wawili hao ni washirika wa Rais Mwai Kibaki, ambaye alitoa wito kwa wananchi kuwa watulivu baada ya ICC kuthibitisha mashtaka yake dhidi ya watu hao.
Wanaharakati wamekuwa wakifanya kampeni kwa viongozi hao kuondolewa madarakani.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema haijafahamika bado iwapo Bw Kenyatta ataachana na nia yake ya kuwania urais.
Zaidi ya watu 1,200 waliuawa katika wiki kadhaa za machafuko kati ya Disemba 2007 hadi Februari 2008, huku watu 600,000 wakilazimika kukimbia makazi yao. Wengi bado hawajapata makazi maalum hadi sasa.
Ghasia zilianza baada ya kuzuka mapigano kati ya wafuasi wa wagombea urais Raila Odinga na Mwai Kibaki, na baadaye kufikia kuuana katika misingi ya kikabila.
Waziri wa zamani wa elimu William Ruto na mtangazaji wa redio Joshua arap Sang, ambao walimpinga Bw Kibaki mwaka 2007, pia wanashtakiwa katika kesi nyingine

Alhamisi, 26 Januari 2012

WIZARA YA ARDHI YAMSHUSHUA JUSSA





NewsImages/6214910.jpg
Tibaijuka akifafanua jambo
Mtandao wa ippmedia unaripoti kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemshushua kwa kuweka wazi kuwa mpango wa Tanzania kuuomba Umoja wa Mataifa (UN).
Kuiongezea maili 150 sawa na kilometa 241.5, kutoka usawa wa mwambao wa Tanzania, haukufanywa na wizara yake peke yake bali una baraka zote za Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Profesa Tibaijuka alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ameshangazwa na taarifa zilizotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti kwamba Serikali ya Tanzania imefanya makosa kuandaa, kupeleka maombi ya kutaka kuongezewa mipaka ya eneo tengefu la bahari kuu (EEZ) bila kuishirikisha Zanzibar.

“Hili suala sijaliamua mimi wala wizara yangu peke yake, lakini nashangaa taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kwamba nimefanya makosa, nisingeweza kwenda mimi bila Mkuu wa nchi kujua na kukubali. Pia tulikuwa na ujumbe kutoka Zanzibar tuliokwenda nao kwa hiyo nashangaa wanaosema hatujashirikisha Zanzibar,” alisema.

Profesa Tibaijuka alisema Tanzania iliingia mkataba na Serikali ya Norway katika kufadhili mradi huo ambapo kulikuwa na wawakilishi kutoka Zanzibar. Aliwataja wawakilishi hao kuwa ni Ayoub Mohamed Mahmoud, ambaye alisema alishiriki kikamilifu katika ziara ya Norway na alipewa nafasi ya kuongea kwa niaba ya SMZ na Zakia Meghji.

“Kwa hiyo madai ya Chama cha Wananchi (CUF) kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushiriki au kushirikishwa hayaendani na yaliyojiri na hayana ukweli wowote,” alisema Profesa Tibaijuka

PICHA YA LEO; TIMU YA TAIFA YA TANZANIA YACHEZA BILA JEZI MBELE YA RAIS WA SUDAN NA TANZANIA MIAKA YA 1970.

Inasemekana toka siku hii Rais Julius Nyerere wa Tanzania hakuingia tena kwenye mechi za mpira wa miguu kutokana na aibu ya maandalizi mabovu ya kushindwa kununua hata jezi kwenye mechi ya kimataifa kama hii, hapa anaonekana Rais Nimeir wa Sudan akiikagua timu ya Taifa Stars huku wachezaji wake wakiwa vifua wazi, je unaikumbuka siku hii illikuwa lini? Tujulishe kwa anuani hiyo hapo juu.

Jumanne, 24 Januari 2012

TAKUKURU YAICHUNGUZA SIMBA NA YANGA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) sasa imenyoosha makucha yake michezoni kwa kuivalia njuga kashfa ya upangaji wa matokeo ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga.



 
PCCB Chief, Edward Hoseah.


Jaribio hilo lakupanga matokeo lilifanyika siku chache kabla Simba na Yanga hazijakutana katika mechi ya mzunguko wa Kwanza Tanzania Bara iliyofanyika Oktoba 29, 2011 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi hiyo Yanga ilishinda 1-0.

Habari za uchunguzi zinaeleza kwamba tayari Takukuru imekwishawahoji watu kadhaa akiwemo kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Simba (jina linahifadhiwa) na wachezaji wa Yanga, wiki iliyopita.

Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, alithibitisha kuwa suala hilo lilikuwa mezani kwao ingawa hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na uchunguzi wao.
“Suala hilo lipo mikononi mwetu linafanyiwa kazi, upelelezi ukikamilika tutatoa tamko,” alisema.

Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba upelelezi unamlenga zaidi kiongozi huyo wa Simba anayedaiwa kumpigia simu mshambuliaji wa Yanga, Pius Kisambale, siku chache kabla ya pambano lao wakati Yanga ikiwa kambini kwenye Hoteli Double Tree iliyoko Masaki, jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema, wakati Kisambale anapigiwa simu alikuwa na baadhi ya viongozi wa Yanga na kwamba simu hiyo iliwashtua viongozi hao, hivyo kumfanya mchezaji huyo aongeze sauti ili nao wasikie kilichozungumzwa.

Shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mshambuliaji huyo alirekodi maneno ya kiongozi huyo mzito wa Simba, kitendo ambacho pia kilifanywa na viongozi waliokuwa wamemzingira.

Katika mazungumzo hayo, inaelezwa kwamba kiongozi huyo wa Simba alimtaka Kisambale acheze chini ya kiwango ikiwa atapangwa na kuahidi kumpatia ‘mzigo’ huku akimwomba awaeleze na wenzake juu ya mpango huo.

Hali hiyo inaelezwa kuwakasirisha viongozi wa Yanga walioamua kulipeleka suala hilo Takukuru ili mhusika achukuliwe hatua za kisheria.

Taarifa zaidi zinasema wiki iliyopita Takukuru ilimhoji Kisambale na wachezaji kadhaa wa Yanga katika ofisi yao iliyoko Upanga jijini dare s Salaam.

Mbali ya Kisambale, kiongozi huyo wa Simba pia amehojiwa na Takukuru kuhusu kashfa hiyo inayoonyesha kukubuhu kwa vitendo vya rushwa michezoni kiasi cha kuporomosha kandanda nchini.

“Rushwa imetawala michezoni na watu wanalichukulia kama shamba la bibi bila kujali namna kiwango cha michezo kinavyoporomoka. Sasa watu wamechoka,” kilisema chanzo hicho.

Kisambale aligoma kuzungumzia suala hilo na kusema hafamu chochote, huku Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akiruka kimanga na kusema hawezi kulizungumzia.

“Siwezi kuzungumzia,nendeni mkamuulize huyo kiongozi wa Simba mwenyewe, mambo haya yako kwenye vyombo vya sheria,” alisema.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa upelelezi umehusisha mawasiliano mbalimbali ya simu kati ya wachezaji wa Yanga na kigogo huyo wa Simba huku taarifa nyingine zikiongeza kwamba hata mawasiliano baina ya kiongozi huyo na baadhi ya waandishi wa habari za michezo nayo yanachunguzwa.

Mbali ya suala hilo, Takukuru pia inadaiwa kuchunguza kashfa inayomhusisha mshambuliaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe aliyetaka kumhonga kipa wa zamani wa Mtibwa, Shabaan Kado katika msimu wa 2010/2011.

Ulimboka alikamatwa na walinzi wa kiwanda cha sukari Mtibwa akiwa na fedha zinazodaiwa zilikuwa rushwa kwenda kwa Kado ili aachie mabao katika mechi yao ya Ligi Kuu.

Vyanzo vya habari vinasema tayari Kado anayeidakia Yanga kwa sasa, amekwishahojiwa na Takukuru, ingawa mwenyewe amegoma kuzungumzia kilichoendelea kwenye mahojiano hayo.

Matokeo ya uchunguzi huo yanaweza kubadili sura ya soka la Tanzania ambalo kwa miaka kadhaa limekumbwa na kashfa nyingi za rushwa, upangaji wa matokeo na uamuzi mbovu, hasa likizihusisha timu za Simba na Yanga


Source: http://www.wavuti.com/

Jumatatu, 23 Januari 2012

DK. SLAA USO KWA USO NA DK. KIKWETE, ILIKUWA JUZI IKULU YA DAR KATIKA MAZUNGUMZO YA KATIBA MPYA.

Mheshimiwa Rais Kikwete akisalimiana na Dk. Slaa juzi usiku Ikulu alipowakaribisha viongozi wa CHADEMA kwa mazungumzo mafupi juu ya Katiba mpya
.
RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mkutano huo ulifanyika jana kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.

Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.

Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Dk Slaa, ambaye alikataa kuyatambua matokeo hayo, tangu wakati huo hawakuwahi kukutana rasmi na Rais Kikwete huku uvumi ukizagaa kwamba  kwamba mwanasiasa huyo amekuwa akijaribu kukwepa asikutane ana kwa ana na Rais Kikwete kwenye mazingira yoyote.

Katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala, hivi karibuni Dk Slaa alidaiwa kumkwepa Rais Kikwete, kwa kutokwenda kukaa kwenye nafasi aliyoandaliwa jirani na kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Ilidfaiwa kuwa nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalumu kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alidaiwa kukikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kukaliwa na mtu.

Hata hivyo Dk Slaa alikanusha uvumi huo na kudai kwamba asingeweza kwenda kukaa jukwaa alilokaa Rais Kikwete kwani yeye si kiongozi wa serikali hivyo kwa mujibu wa itifaki, asingeweza kumfuata Rais Kikwete na kwenda kumsalimia alipoketi.

Hii ni  mara ya pili kwa ujumbe wa Chadema kukutana na Rais Kikwete Ikulu  kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya

Jumapili, 22 Januari 2012

IJUE RATIBA YA KOMBE LA MATAIFA HURU YA AFRIKA YALIYOANZA KUTIMUA VUMBI JANA.


Wizard: Morocco forward Adel Taarabt
Wizard: Morocco forward Adel Taarabt

GROUP A
Jan 21: Bata, Equatorial Guinea
Equatorial Guinea vs. Libya, 18.30 GMT
Senegal vs. Zambia, 2100 GMT

Jan 25: Bata, Equatorial Guinea
Libya vs. Zambia, 1600 GMT
Equatorial Guinea vs. Senegal, 1900 GMT

Jan 29: Malabo, Equatorial Guinea
Equatorial Guinea vs. Zambia, 1700 GMT
Bata, Equatorial Guinea
Libya vs. Senegal, 1700 GMT
GROUP B
Jan 22: Malabo, Equatorial Guinea
Ivory Coast vs. Sudan, 1600 GMT
Burkina Faso vs. Angola, 1900 GMT
Jan 26: Malabo, Equatorial Guinea
Sudan vs. Angola, 1600 GMT
Ivory Coast vs. Burkina Faso, 1900 GMT
Jan 30: Bata, Equatorial Guinea
Sudan vs. Burkina Faso, 1800 GMT
Malabo, Equatorial Guinea
Ivory Coast vs. Angola, 1800 GMT
GROUP C
Jan 23: Libreville, Gabon
Gabon vs. Niger, 1600 GMT
Morocco vs. Tunisia, 1900 GMT

Jan 27: Libreville, Gabon
Niger vs. Tunisia, 1600 GMT
Gabon vs. Morocco, 1900 GMT

Jan 31: Franceville, Gabon
Gabon vs. Tunisia, 1800 GMT
Libreville, Gabon
Niger vs. Morocco, 1800 GMT
GROUP D
Jan 24: Franceville, Gabon
Ghana vs. Botswana, 1600 GMT
Mali vs. Guinea, 1900 GMT
Jan 28: Franceville, Gabon
Botswana vs. Guinea, 1600 GMT
Ghana vs. Mali, 1900 GMT
Feb 1: Libreville, Gabon
Botswana vs. Mali, 1800 GMT
Franceville, Gabon
Ghana vs. Guinea, 1800 GMT

 
QUARTER-FINALS
Feb 4, Match 25, Bata, Equatorial Guinea
Group A winner vs. Group B runner-up, 1600 GMT
Match 26, Malabo, Equatorial Guinea
Group B winner vs. Group A runner-up, 1900 GMT
Feb 5, Match 27, Libreville, Gabon
Group C winner vs. Group D runner-up, 1600 GMT
Match 28, Franceville, Gabon
Group D winner vs. Group C runner-up, 1900 GMT
SEMI-FINALS
Feb 8, Bata, Equatorial Guinea
Match 25 winner vs. Match 28 winner, 1600 GMT
Libreville, Gabon
Match 27 winner vs. Match 26 winner, 1900 GMT
THIRD PLACE
Feb 11, Malabo, Equatorial Guinea, 1900 GMT
FINAL
Feb 12, Libreville, Gabon, 1900 GMT

MANCHESTER UNITED YAIVUTA SHATI MANCHESTER CITY

 .
Picha na makataba yetu

Mwanzoni mwa mechi hii United ilikua nyuma kwa pointi sita baada ya Manchester City kuirarua Tottenham hotspurs 3-2 kwenye uwanja wa Ettihad mapema siku ya jumapili.
Manchester United iliongoza kwa bao la Antonio Valencia dakika moja kabla ya kipenga cha mapumziko kuipa klabu yake bao 1-0. Bao hilo lilifutwa na la nahodha wa Arsenal katika kipindi cha pili na kuonekana kama liliowaamsha wachezaji wa Arsenal.
Mabadiliko yaliyofanywa na pande hizi mbili hayakuonekana kubadili mchezo ingawa wadadisi wengi wanajiuliza sababu iliyomfanya Arsene Wenge kumuondoa mchezaji wake aliyeonyesha mchezo mzuri Alex Oxlade-Chamberlain
Licha ya juhudi na kuonyesha matumaini ya kuongezea mabao kwa Arsenal Manchester United ikitumia uzowefu wake na kuzingatia mpango wake waliokuja nao waliendelea kuizuia Arsenal isifurukute na kama ilivyo tabia yao ya kukamilisha tamaa yao dakika za mwisho,zikisalia dakika tisa kabla ya kumalizika kwa mechi Danny Welbeck akatikisa nyavu za Arsenal na kuipatia ushindi na pointi tatu. Arsenal 1 Manchester United 2

MKE WA MTU SUMU, DEREVA WA BODABODA AFUMANIWA NA KUUWAWA KIKATILI HUKO MPANDA.

DEREVA wa pikipiki za kukodi maarufu kama 'bodaboda', Mussa Kimbei (43), ameuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke mdogo wa mfanyakazi wake.
Dereva bodaboda wa Uganda(picha na maktaba)

Inadaiwa kuwa marehemu ambaye ni mkazi wa eneo la Kichangani mjini Mpanda alikuwa pia akimiliki shamba la tumbaku ekari nane na ekari nne za shamba la mahindi katika Kijiji cha Kambanga ambapo aliajiri walinzi na vibarua wanane.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, mauaji hayo yalitokea
juzi saa tano usiku shambani kwa marehemu katika kitongoji hicho cha Kambanga baada ya
kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa msimamizi wa shamba lake aitwaye Christopher
Bonge.

Mantage alisema mbali ya kumuua kikatili kwa kumcharanga vipande vipande kichwa kwa
mapanga, wananchi hao walichoma moto vibanda vitatu vya kukaushia tumbaku na kufyeka
mashamba yake ya tumbaku na mahindi kisha wakateketeza pikipiki yake kwa moto.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, baadhi
ya madereva wa bodaboda ambao wanadai kuwa marafiki wa karibu wa Kimbei, wanadai kwa muda mrefu Kimbei alikuwa akituhumiwa kufanya mapenzi na wake za wanakijiji hao wa Kambaga.

“Kimbei ambaye ameacha wake wawili na watoto tisa, inadaiwa alikuwa akitumia fedha zake baada ya mauzo ya tumbaku kurubuni wake za wanakijiji hao. Huyu mke mdogo wa msimamizi wa shamba lake walikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu,” alisema mmoja wa madereva hao.

DUKA LA VINYWAJI BARIDI LANUSURIKA KUUNGUA MOTO STENDI YA MABASI NACHINGWEA JANA USIKU.


Viti vya plastiki vilivyoungua ndio bidhaa pekee iliyoathirika na moto huo.

Kumekuwa na tabia au dhana ya kulitaja sana Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa linahusika sana na kusababisha moto sehemu mbalimbali, lakini jana Mambobado ilishuhudia moto katika moja ya vibanda vya biashara kuzunguka Stendi kuu ya mabasi Nachingwea mida ya saa tano usiku uliosababishwa na mkaa wa moto uliohifadhiwa ndani ya kibanda hicho kwa ajili ya matumizi ya siku inayofuata.

Wasamaria wema wakishuhudia tukio hilo mara baada ya kuzimwa kwa moto huo ambao ulisababisha hasara kidogo maana ulizimwa kabla haujakolea na pengine kuhamia vibanda vingine. Ilibidi wasamaria wema wavunje mlango huo baada ya kusikia harufu ya vitu vinavyoungua na mwanga wa moto kuonekana kwa ndani, mwenye mali alijulishwa baadae na alikuta vitu vyake salama.

Jumamosi, 21 Januari 2012

WATEJA WA M-PESA WENYE AKAUNTI CRDB SASA KUWEKA NA KUTOA FEDHA KUPITIA SIMU YA MKONONI




















Wateja wa Vodacom M-PESA wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-PESA.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB..
Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki.
“Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.
Huduma ya Vodacom M-PESA ya kwanza sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza nchini ni kielelezo makini cha ubunifu na namna ambavyo Vodacom imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya simu za mkononi.
Ikiwa na mawakala zaidi 20,000 nchi nzima M-PESA inabakia kuwa huduma salama zaidi, ya haraka, uhakika na yenye kuaminika kwa ajli ya kuweka na kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na manunuzi mbalimbali, kulipia kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya sabini na tano ulimwenguni.
“Hakuna mteja wa Vodacom M-pesa atakaesimama kwenye foleni au kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata tawi la benki yake ya CRDB, sasa wataweka na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote bila kuathiri shughuli nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha yamekuwa rahisi zaidi.”Aliongeza Bw. Rene
Tangu ilipoanzishwa mwaka 2007, huduma ya Vodacom M-PESA imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa huduma yenye usalam zaidi, yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini na hivyo kuchangia maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya wananachi kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo
    1. Piga *150#
    2. Chagua kulipia bili
    3. Ingiza namabri ya biashara ambayo ni 900500
    4. Ingiza nambari ya kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
    5. Weka kiasi cha fedha mteja anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
    6. Ingiza nambari ya siri.
    7. Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.
Baada ya hatua hizi mteja atapokea mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na baada ya dakika 8 atapokea ujumbe kutoka benki ya CRDB.
Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo
      1. Piga *150*03#
      2. Ingzia nambari ya siri
      3. Chagua nambari 3 (Hamisha fedha)
      4. Chagua nambari 3 (M-PESA)
      5. Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
      6. Thibitisha nambari yako ya simu
      7. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
      8. Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.
        Ili kuwa na uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.
Usajili huo hufanyika MARA MOJA TU na kwamba unaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*03# na maelezo ya namna ya kujisajili yatatotekea ambayo mteja atapaswa kuyafuata.

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU MBILI WILAYANI NACHINGWEA, AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal akifunua kitambaa kuashiriwa kuzinduliwa kwa Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Nachingwea hapo jana, alikuwa katika ziara ya siku mbili wilayani Nachingwea kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji safi ujulikanao kama Mbwinji iinaotarajia kukamilika hivi karibuni unaojengwa na Wachina.
Kikundi cha ngoma kikifanya mazoezi ya kujiandaa kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais hajawasili katika viwanja hivyo vya shule mpya ya Wasichana Nachingwea.
Wananchi wakisubiri kumsikiliza mgeni rasmi katika maeneo ya shule hiyo jana, leo amemaliza ziara yake hapa na ameelekea wilaya ya Lindi kwa ziara kama hiyo.

PICHA YA LEO; KWA WALE WALOSOMA ZAMANI "SIZITAKI MBICHI HIZI" KISWAHILI DARASA LA TATU AU NNE!!!!?

Kwa taarifa hii picha ilikuwa inapatikana kwenye kitabu cha Kiswahili kilichokuwa kinaitwa "Tujifunze Lugha Yetu-5" ambapo kulikuwa na sura moja ina shairi lililoitwa Sizitaki Mbichi Hizi. Ukweli vitabu vile vilikuwa na mafundisho bora sana kwa watoto kwa hadithi zake zenye kuvutia.

TAMKO LA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIISLAMU TANZANIA

IN THE NAME OF ALLAH, THE ALL-COMPASSIONATE, ALL - MERCIFUL
TANZANIA MUSLIM STUDENTS AND YOUTH ASSOCIATION (TAMSYA)
HEAD OFFICE
P.O BOX 35491,
DAR ES SALAAM
TANZANIA –EAST AFRICA 
Website: www.tamsya.org Email: info@tamsya.org
Phone: +255732994703 Fax: +255732994703 Mobile: +255715 944514
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NDUGU WANAHABARI
Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote. Pili tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa na majukumu mengi ya kutoa taarifa kwa wananchi.Kwa mara ya kwanza tumeamua kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ili muifikishe kwa Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusieni
juu ya ukweli na uaminifu katika kuripoti taarifa hii.Tuna kuusieni tena kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa.Kutakuwa na nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayo haikueleweka.

NDUGU WANAHABARI
Tuliowaita ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Tanzania yaani Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA).Jumuiya yetu inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuata sheria za nchi.

NDUGU WANAHABARI
Jumuiya yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunzi wafuasi wa dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati na vyuo vikuu na vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.

NDUGU WANAHABARI
Tumeamua kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapata wanafunzi waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa muda mrefu. Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katika masomo yao pindi wakiwapo shuleni.

NDUGU WANAHABARI
Sheria ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibu wa dini yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini nakuswali tu bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada ni kila jambo analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungu likiwa katika muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.

NDUGU WANAHABARI
Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa
HIJABU shuleni,,Tumepata mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu za kusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na vyuo. Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya shule katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafali zinapangwa kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihanivyuo vikuu hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa
kusimama mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.

Wanafunzi waislamu wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada ya muda wa masomo katika shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda
na Rozari masaa 24. Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo
kwenda kufundisha baibal knowledge.

Vipindi vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba
mchana siku ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa
kuenda msikitini kwa ajili ya swala ijumaa.

NDUGU WANAHABARI
Tutatoa mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislam
wamefanyiwa madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na
kutukaniwa Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA
imefuatilia bila ya mafanikio.

SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO
Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa
shule.

Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo
ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya
Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupigapicha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya
namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na
haukuagiza hivyo.


SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO
Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. 

Lakini
sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda, Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.

SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa
tuliyo letewa ya 17/03/2011.

SHULE YA SEKONDARI LUGOBA
Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.

Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.

Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya nkuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa
na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.

SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA
Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.

SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA
Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.

Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha
kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo.

Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.

Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.

Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu
kama kanzu kuwa ni Mashoga

NDUGU WANAHABARI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM) ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia
njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya
kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.

NDUGU WANAHABARI
Tukio kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao
wanatarajiwa kufanya mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili.

Aidha wengine waliosalimika kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu
ya kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongoni
mwa masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti
ambalo linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.
Sababu na kosa la kufukuzwa wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba
uongozi wa shule uwape eneo maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama
vile walivyotengenezewa wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo,
kulalamika lugha za kashfa na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa
shule dhidi ya wanafunzi wa kiislamu uislamu shuleni hapo.

Kilichowaponza wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na
upendeleo kwa wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule
kuteua viongozi wa serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa
wakirsto huku wakitoka nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad
ameshindwa katika uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya
yamefanyika mkuu wa shule akiyaona bila ya hata kukemea na
kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa
ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.

NDUGU WANAHABARI
TAMSYA mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya
jitihada mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husika katika kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.

Pia walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya
mbali kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote, na wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari palen alipopinga dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislamshuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim
wa kikristo.

NDUGU WANAHABARI
Hapa tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania anajua haya hata watu wa kawaida pia
.
Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa serikali mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa
waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali
ni tatizo la kihistoria.

Sisi wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidin kuwa hili si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na kuwakandamiza waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi
zilizotumiwa na uongozi wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo katika sekta zote za elimu nchini.

Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini (20) wa kiislam na wengine
  
kuwekewa masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe
kurudi shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo
walifanyiwa babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha
kuacha dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani
walifanya maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini
yao kwani kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa
katika dini ya haki ya uislam.

Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu Tunasema kusoma ni sehemu ya dini yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa
kabisa.

Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha wito wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.

NDUGU WANAHABARI
Kadhia ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika wizara ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake. Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya bodi ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza
kuwa amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya kuwaruhusu kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.

Hukumu hii haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa kuwasikiliza hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru
wa imani na kuabudu.

Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya yanayoendelea kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama
wanajamii wengine.

Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya
mambo yafuatayoTunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na
wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe
13/01/2012.

Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata
wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.

Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.

Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.

Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa ajili ya watu wa dini zote. Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo, hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.

Kila jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kamawanafunzi daraja la pili katika nchi yetu.
Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi tunalazimika kupaza sauti zetu kwa kuingia barabarani kuonesha hisia zetu katika hali ya unyonge wetu

NDUGU WANAHABARI
Tunakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi haitokoma.Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya.

Tunasema “tumenyanyaswa,tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na mavyuoni.”

Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru, wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia hii serikali na jamii itasikia kilio chetu.

 ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANIWOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.

Ahsanteni. 

JAFARI SAIDI MNEKE 
RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA
WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)

Jumatano, 18 Januari 2012

R.I.P MBUNGE MTEMA- AMEZIKWA LEO HUKO IFAKARA



Marehemu Mtema akiagwa leo wakati ya misa ya mazishi huko Ifakara.
Naibu Spika, Job Ngugai (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Kiongozi wa Kambi ya Upinzania na Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Zitto Kabwe wakifuatilia kwa makini Misa Maalum ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Marehemu Regia Mtema Ifakara leo.…
credits; globalpublishers.info

MADAKTARI WA MAZOEZI MUHIMBILI WALIPWA MADAI YAO, SERIKALI YAITOLEA UVIVU MAT.

SERIKALI imewalipa madai yao yote madaktari waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Sehemu ya moja ya majengo ya Hospitali ya Rufaa Muhimbili

Fedha zilizolipwa ni jumla ya Sh milioni 826. Lakini pia imewataka madaktari wanachama wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa kiapo na kuachana na uanaharakati.

Aidha, imewataka madaktari bingwa 51 ambao hawajaripoti katika vituo vyao vya kazi katika hospitali za rufaa za mikoa na manispaa za Dar es Salaam, kufanya hivyo mara moja, wakitambua kuwa walisomeshwa na fedha za walipa kodi.

MAT pia imetakiwa kutambua kuwa uanachama katika chama hicho ni wa hiari na kwamba Mganga Mkuu nchini, Deo Mtasiwa, hataondolewa katika wadhifa huo kama madaktari hao wanavyotaka.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia suala la madaktari walio katika mazoezi ya uboreshaji wa taaluma kwa vitendo Muhimbili.

Alisema hivi karibuni wataalamu 195 waliokuwa mazoezini Muhimbili waliamua kutoendelea na ratiba zao za mazoezi kwa vitendo hadi watakapolipwa posho zao za Novemba na Desemba mwaka jana. Wamelipwa jumla ya Sh milioni 826.

“Tatizo lilitokea baada ya kuchelewa kutolewa kwa fedha za posho kwa wataalamu wa sekta ya afya, Wizara ilihakikisha fedha zinapatikana haraka na wakati huo huo ikiwasiliana na wawakilishi wa wataalamu hao na uongozi wa taasisi walizokuwa wakifanyia mazoezi kuhusu jitihada zinazofanywa kutatua tatizo hilo,” alisema Dk. Nkya.

Aidha, alisema pamoja na Wizara kuwahakikishia wataalamu hao kuwa suala hilo limepatiwa ufumbuzi, bado walishikilia msimamo wa kutorudi vituoni mpaka wapokee fedha, kitendo ambacho hakikuwa cha kiungwana.

Dk. Nkya alisema baada ya hali hiyo, Wizara ilipeleka wataalamu 51 waliokuwa wakisubiri kuanza mafunzo Januari mwaka huu, ili kuchukua nafasi za wataalamu waliokataa kurejea, ili kuzuia athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa wagonjwa. Wataalamu 60 hawakushiriki mgomo huo.

Alisema kitendo cha wataalamu hao kutoendelea na mazoezi kilisababisha uongozi wa Muhimbili kuwaandikia barua za kuwarudisha wizarani ambako ndiko ombi la kuitaka hospitali hiyo kuwapa nafasi za mazoezi lilitoka.

Jumanne, 17 Januari 2012

WANAKIJIJI WA IKUNGU WILAYANI NACHINGWEA WALALAMIKIA MWEKEZAJI ANACHAFUA MAZINGIRA KWA MADAWA YA SUMU KALI.

Kampuni inayojishughulisha na uchakachuaji wa mchanga uliobakizwa baada ya kuondoa dhahabu ijulikanayo kwa jina moja tu la MANJANJO iliyopo maeneo ya mlima Ikungu wilayani Nachingwea mkoani Lindi inalalamikiwa na wanakijiji kuwa inachafua mazingira pale dawa aina ya CYNADE inayotumika kukamata dhahabu katika hali ya kimiminika inapoingia katika vyanzo vya maji hasa wakati huu wa mvua za masika. Hali hii imezua sintofahamu kwa uongozi wa kijiji na wanakijiji halikadhalika na kupelekea wananchi kutaka Kampuni hiyo ifukuzwe kabisa eneo hilo.
Mambobado ilipata nafasi ya kutembelea eneo la mgodi ikiambatana na uongozi wa serikali ya wilaya na wawakilishi wa uongozi wa kijiji cha Ikungu ili kujionea hali halisi baada ya madai kuwa baadhi ya mbuzi walikufa baada ya kunywa maji yaliyochanganyika na dawa yenye sumu mara baada ya mkutano na wanakijiji na serikali yao ambayo wajumbe asilimia 90 walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao kwa vile serikali haisikilizi kilio chao wakati wanaathirika na sumu. Tukiongea na mkemia wa kampuni hiyo alisema kuwa madai kuwa mbuzi wamekufa na dawa kuingia kwenye mkondo wa maji si kweli ila ni chuki za kisiasa kati ya wanakijiji kwa kulishana maneno ya uwongo ili waichukie kampuni yao.
Aliendelea kusema kuwa wao huvundika udongo uliotumika na wachimbaji wengine kama picha ya juu inavyoonesha na baadae huchanganya na maji yenye dawa iitwayo CYNADE katika mashimo maalumu yaliyojengewa kwa simenti pembeni ambapo dhahabu isiyoonekana kwa macho hujichanganya na maji yenye dawa na kuingia eneo maalumu kama inavyoonekana picha hii ya juu ambapo baadae huchangayika na makaa ya mawe na kukusanywa katika viroba na kupelekwa Mwanza kwa ajili ya kuchomwa ili kupata dhahabu halisi.
Hapa ndipo dhahabu huchanganyika na makaa ya mawe na kuopolewa tayari kwenda kuchomwa Mwanza ili kutenganisha makaa na dhahabu, baadae maji yenye dawa iliyopoa hurudishwa tena kwenye mzunguko wa kwanza na kuongezwa dawa tena iwapo imepungua. Mtaalamu alisema maji haya yaliyotumika hawayaachii ila wanayatumia tena na hayana madhara isipokuwa katika hatua ya mwanzo kabla hayajatumika, aliyashika maji haya na kunawa ingawa alisema yana madhara iwapo yataingia machoni, mdomoni au kwenye vinyweleo ambapo huduma ya kwanza itatakiwa ili kuzuia madhara.
Hapa ni maji yaliyojichuja toka kwenye udongo uliotumika na kuchanganyika na maji ya mvua ambapo walionekana vyura ndani yake wakicheza kwa maana kuwa hayana sumu, pamoja na hayo hakuna maji yanayoachiwa kuingia kwenye mkondo wa maji. Watalamu wa mazingira wametaarifiwa  pamoja na wale wa madini ili waje kutatua mgogoro huu, Afisa Afya pia ametoa maelekezo ya nini kifanyike ili kuboresha miundombinu.





Jumatatu, 16 Januari 2012

REGIA MTEMA KUAGWA KESHO KARIMJEE

Mbunge huyo alifariki juzi saa 5:15 baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika eneo la Ruvu JKT, mkoani Pwani baada ya gari alilokua akiendesha kupinduka zaidi ya mara mbili.
Gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha Mh. Mtema
Taarifa zilizotolewa na jeshi la polisi mkoani humo zilisema , marehemu Mtema alikuwa akiendesha gari aina ya LandCruiser namba T 296 BSM alipokuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Pwani.
Taarifa hiyo ilisema akiwa akiendesha gari hilo alipofika eneo hilo alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake lakini alishindwa kufanya hivyo ndipo gari lake lilipopinduka na kusababisha kifo chake.




Mh, Regia Mtema enzi za uhai wake.
Alisema Mtema alikuwa akiendesha gari aina ya Landcruiser lenye namba T 296 BSM, akitokea Dar es Salaam kuelekea Chalinze.
Taarifa zaidi zilieleza kwamba Mtema alikuwa anakwenda kukagua kiwanja chake mkoani humo na umauti kumfika njiani, pia marehehmu ameacha pacha wake ambaye alinusuruka na kifo hicho muda mchache tu alipomshusha pacha wake.
Mwili huo unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee na kuzikwa keshokutwa huko Ifakara nyumbani kwao

Alhamisi, 12 Januari 2012

MASHAUZI CLASSIC YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA NACHINGWEA, WACHEZA TAARAB KWENYE MVUA.

Isha Mashauzi akiwajibika stejini juzi jumatatu. Licha ya mvua kubwa kunyesha mashabiki waliendelea kucheza bila kujali hali hiyo.

MESSI AIBUKA MCHEZAJI BORA WA DUNIA MWAKA 2011.


Lionel Messi ameshinda tuzo ya Fifa ya mwanasoka bora wa mwaka 2011 ya Ballon d'Or, na kuwa mchezaji wa nne katika historia duniani kushinda tuzo hiyo mara tatu. Mshambuliaji huyo kutoka Argentina mwenye umri wa miaka 24, aliwashinda Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na mchezaji mwenzake wa Barcelona, Xavi.  Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson alishinda tuzo ya huduma kwa soka, huku meneja wa Messi, Pep Guardiola akipata tuzo ya kocha bora wa mwaka. Messi, ambaye aliwahi pia kushinda tuzo hiyo yenye hadhi mwaka 2009 na 2010, alikuwa mchezaji bora katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2011, dhidi ya Manchester United, na pia alishinda ligi ya Uhispania, kombe la Supercopa la Uhispania, Kombe la Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la klabu mwaka jana

LEO NI KUMBUKIZI YA MIAKA 48 YA MAPINDUZI TUKUFU YA ZANZIBAR.

Mzee Hassan Nassor Moyo, mmoja wa Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 1964.

WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, BADO WAPO BARABARANI KWA NINI!!!? SERIKALI ICHUKUE HATUA KWANI FEDHA ZA MAAFA ZIPO.

Baadhi ya waathirika wa mafuriko wanaoishi nje ya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa wakiwa na watoto wao kama walivyokutwa kando ya barabara ya Uhuru Dar es Salaam. Kushoto ni Mwanaharusi Abubakari, Zarika Juma, Fatuma Hemedi na Mwajabu Haruna. Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Waathirika waliokuwa wapangaji wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, Eziaka Wema, eneo hilo lina jumla ya waathirika 130 ambao hawana mahali pa kuishi. (Picha na Mohamed Mambo)

Jumatatu, 9 Januari 2012

PICHA YA LEO;WANAJUA MADHARA YAKE!!?

Picture
Wananchi wakiwania kuchota mafuta toka katika gari ya mafuta iliyoaguka huko Iringa maeneo ya Ihemi  barabara ya Mbeya -Dar es salaam.
Picture
Walinda usalama nao walikuwepo lakini hawakuchukua hatua yoyote, hatujifunzi kutokana na makosa kwa nini!!? Picha toka francis gordwin blog.

MASHAUZI CLASSIC TAARAB KUTUMBUIZA NDANI YA NACHINGWEA LEO USIKU.

Isha Ramadhan a.k.a Mashauzi Original, ndiye kiongozi wa kundi hilo la Taarab, tayari yupo Nachingwea kwa shoo ya usiku wa leo.
Mtoto anavutia ile mbaya, uongo!!!? Kama kawaida show itafanyika katika ukumbi maarufu wa NR.
Isha Ramadhani. Mkurya wa kwanza kuimba taarabu.

Jumapili, 8 Januari 2012

CHAZ BABA AIHAMA TWANGA PEPETA, HUENDA AKAJIUNGA NA MAPACHA WATATU.



NewsImages/6172494.jpg
Charles Gabriel au maarufu kwa jina la 'Chaz Baba'
Mwimbaji wa kutumainiwa wa bendi ya muziki wa dansi ya The African Stars 'Twanga Pepeta' Charles Gabriel au maarufu kwa jina la 'Chaz Baba' ametangaza kujitoa katika bendi hiyo na kufanya shughuli zake mwenyewe.
Chaz Baba alitangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa kujitoa kwake Twanga Pepeta kumetokana na mambo mengi mojawapo ni kutokuwa na mkataba wa kazi.

Alisema tangu ajiunge na bendi hiyo mwaka 2005 hajawahi kupewa mkataba wowote wa kazi zaidi ya kulipwa mshahara tu kitu ambacho amekiona kama ni kinyume na utaratibu wa kazi.

Chaz Baba aliongeza kuwa kuanzia sasa atakuwa chini ya meneja wake aliyemtaja kwa jina la Benard Msekwa.

“Kwa sasa nitakuwa nasimamiwa na meneja wangu mpya (Msekwa) hivyo kila kitu kinachohusu masuala yangu ya kazi ama ya kisanii kwa ujumla kitakuwa chini yake, kama ni onyesho ama kuhamia bendi nyingine yeyote ni juu yake", alisema Chaz Baba.

Aidha mwimbaji huyo maarufu aliongeza kuwa baada ya kujitoa Twanga Pepeta anatarajia kuzindua albamu yake binafsi yenye nyimbo nane.

"Mpaka sasa nimeishakamilisha vibao kama sita hivi hivyo katika miezi ya karibuni nadhani albamu nzima itakuwa imekamilika", alisema Chaz Baba.

Alizitaja baadhi ya nyimbo kwenye albamu yake kuwa ni pamoja na "Nusu Chizi" ambayo amewashirikisha "Mapacha Watatu" na nyimbo zingine kama vile "Blandina", "Papa Fred", "Mayasa" na "Ninaelekea wapi".