Jumatatu, 24 Juni 2013

VIJANA WA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA WAMEHITIMU MAFUNZO JANA KAMBI YA MLALE SONGEA.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akisalimiana na Makamanda wa JKT Mlale juzi jumamosi alipoenda kufunga mafunzo ya vijana wapatao 370 toka mashuleni.

Askari waliohitimu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi mara baada ya kumaliza gwaride lao la maonesho. Ni miaka 19 imepita tangu mafunzo haya yalipositishwa na serikali kwa sababu ambazo haziko wazi hadi yalipoibuliwa tena mwaka huu, mafunzo haya ni muhimu katika kujenga nidhamu na moyo wa uzalendo kwa vijana wetu.
(Picha by Tetez)

Jumamosi, 22 Juni 2013

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE PAMOJA NA FAMILIA YAKE WAHUDHURIA MAZISHI YA SERGENT DETECTIVE CHRISTOPHER KYENDESYA, HAPO JANA HUKO MBEYA

Marehemu Detective Sergent Christopher pichani enzi za uhai wake

WAKAZI WA MKOA WA RUVUMA HUSUSAN SONGEA MJINI WATAMKUMBUKA ASKARI HUYU MIAKA YA 90 KWA UJASILI WAKE WA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI WAKIWEMO ASKARI POLISI WENZIE NA KUWAWEKA NDANI YA MKONDO WA SHERIA NA KUFIKIA KUPEWA TUZO YEYE NA WENZAKE NA RPC WA WAKATI HUO.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Wa katikati akiwa na Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kushoto pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Diwani Athumani wakiingia katika nyumba ya Mama wa Marehemu kwa ajili ya kuhani Msiba

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji na kumpa pole Mama wa Marehemu Mbunge wa viti Maalum Mama Kyendesya
 Mke wa Rais Mama Salma kikwete akiwapa pole ndugu jamaa na Marafiki
 Kaka wa Muheshimiwa Rais Mzee Miraji Kikwete akimpa pole Mama wa Mareheremu Sargent Christopher Kyendesya
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa salamu zake za


 Kamanda wa Polisi Mkoa Diwani akitoa Salamu za Pole kwa ndugu jamaa na Marafiki kwa Niaba ya Jeshi la Polisi.

 Msemaji Kutoka Jeshi la Polisi na aliyeongoza msafara wa kuuleta mwili wa Marehemu, akisoma Historia fupi ya Marehemu.
 Kaka wa Marehemu Mzee Miraji Kikwete wa Pili kushoto akiwa katika ibada ya Mazishi
Kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mama wa Marehemu Muhemishimiwa Mbunge wa viti maalum mstaafu Mama Kyendesya, Mke wa Marehemu Christopher Kyendesya pamoja na ndugu
 Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Muheshimiwa Abas Kandoro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani pamoja na Mkuu wa usalama Mkoa wa Mbeya
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa Heshima za Mwisho katika Mwili wa Marehemu Sergent Detective Christopher Kyendesya
 Kaka wa Muheshimiwa Rais Jakaya Kikwete , Miraji Kikwete akitoa salamu za mwisho katika  mwili wa Marehemu Sergent Detective Christopher Kyendesya
 Mama wa Marehemu Muheshimiwa Mbunge Mstaafu viti maalum Mama Florence Kyendesya akitoa salamu za mwisho katika  wili wa Marehemu Sergent Detective Christopher Kyendesya
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akitoa salamu za mwisho katika mwili wa Marehemu Sergent Detective Christopher Kyendesya
Wananchi mbalimbali wakiwa katika Mazishi ya Marehemu Sergent Detective Christopher Kyendesya.
 Kazi ya Mazishi ikiwa inaanza
 Salamu za Rambirambi zikitolewa kwa niaba ya Mbunge wa viti Maalum Dr. Mary Mwanjelwa
 Aliyekuwa Mratibu wa Shughuli ya Mazishi Bwana Mwakipesile akizungumza jambo
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha FFU wakifyatua risasi juu ikiwa ni Ishara ya Heshima katika Mazishi hayo
 Mchungaji wa Kanisa la Moraviani akitoa Mbaraka wakati wa kumaliza ibada ya Mazishi

 Mke wa Marehemu Sergent Christopher Kyendesya akiweka Shada la Maua
 Mama wa Marehemu Sergent Christopher Kyendesya , Muheshimiwa Mbunge Mstaafu Florence Kyendesya akiweka Shada la maua katika Kaburi
 Mtoto wa Maremu jina Erick akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba yake pia kwa niaba ya Pacha wake ambaye alichelewa Mazishi
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Akiwa na Kaka wa Muheshimiwa wa Rais Jakaya Kikwete wakiweka Shada la Mauwa katika kaburi la Marehemu Sergent Detective  Christopher Kyendesya
 Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa Abas Kandoro pamoja na Mkewe wakiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani  akiweka shada la maua katika kaburi la maremu kwa niaba ya Jeshi la Polisi

Afisa usalama wa Mkoa akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu
 Ndugu Shitambala wa Pili kutoka Kushoto akiwa katika msiba
 Hawa ni vijana kutoka Sae ambao ndio waliochimba kaburi la Marehemu . 
CREDITS
Picha zote na Mbeya yetu

Jumatatu, 17 Juni 2013

UCHAGUZI MDOGO LINDI. CCM YASHINDA KITI CHA UDIWANI KATA YA STESHENI WILAYANI NACHINGWEA.

Mwenyekiti wa CCM Taifa wa sasa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere enzi hizokatika moja ya mikutano ya Chama
.
Chama cha Mapinduzi jana kimetangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Udiwani wa Kata ya Stesheni  wilayani Nachingwea mkoani Lindi  katika Uchaguzi uliofanyika jana jumapili baada ya mgombea wake kupata kura 806, akifuatiwa na mgombea wa CUF 480, CHADEMA 327  na Chama kipya cha ADC kiliambulia kura 48. CCM imeweza kutetea kiti hiki baada ya aliyekuwa Diwani Bi. Mpoyo kufariki ghafla mwaka jana.

Jumapili, 16 Juni 2013

ALSHABAAB WASHINDWA KUSIMAMIA SHARIAH KAMA WANAVYOJINASIBISHA HASA WANACHAMA WAO WANPOHUSIKA NA HUKUMU HIZO.

Uhalifu wa hivi karibuni wa al-Shabaab unaonyesha upuuzaji wa sharia

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Wanamgambo wa al-Shabaab wamefanya mfululizo wa mashambulio ya ukatili na uhalifu dhidi ya raia katika wiki za hivi karibuni -- utekaji, kukata vichwa na kupora Wasomali katika kupuuza kabisa sheria za sharia ambazo kundi hilo linadai kuzitetea.
  • Askari polisi wa Somalia akisimamia sheria za barabani kwa shughuli zinazoshukiwa za magaidi kwenye eneo la ukaguzi huko Mogadishu. [Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
    Askari polisi wa Somalia akisimamia sheria za barabani kwa shughuli zinazoshukiwa za magaidi kwenye eneo la ukaguzi huko Mogadishu. [Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
Tarehe 30 Mei, al-Shabaab waliagiza kuachiwa kwa wapiganaji wake sita, waliotuhumiwa kwa kupora dola 6,000 kutoka katika duka la dawa huko Baardheere na kuhukumiwa kukatwa mikono yao ya kuume.
"Nilikusanyika na kundi kubwa kutoka mjini kushuhudia adhabu ambayo ingetolewa kwa wapiganaji sita wa al-Shabaab, kwani tulitarajia mikono yao ya kuume kukatwa," alisema Yusra Nur Abdirahman, mwenye umri wa miaka 28 na mkaazi wa Baardheere. "Cha ajabu, mwakilishi kutoka katika kundi hili [aliyekuwa anahusika kutoa hukumu] Shekhe Aadan Nuh alitangaza kwa kutumia kipaaza sauti kwamba wajahidina hao sita wangepigwa viboko 39 kama adhabu ya kosa lao."
Alisema Nuh aliagiza dola 4,900 kurudishwa kwa mfamasia huyo, ambaye ni muungaji mkono al-Shabaab .
"Uamuzi huu wa aibu na wa kuchekesha ambao kwa hakika ulinishangaza na niliuchukulia kama uliokusudiwa kudanganya na kupotosha watu na kuhimiza wanachama wa kikundi hiki kupora mali binafsi na mali za familia," Abdirahman aliiambia Sabahi.
Huu ni mfano tu wa hivi karibuni wa jinsi adhabu za al-Shabaab zisivyo na msingi maalumu na za kinafiki, kwa kuwa wapiganaji walikutwa na hatia ya makosa hawapaswi kuumia na adhabu zilizoagizwa, alisema, akiongeza kwamba wapiganaji pia wameanzisha ulipizaji kisasi dhidi ya raia wa Somalia, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara au kuwakata vichwa ndugu wa viongozi kutoka Gedo na Hiran.
Abdirahman aliviomba vikosi vya serikali ya Somalia kukomesha vitendo vya kutisha vya al-Shabaabvya kuteka nyara, kuua, kutesa na kupiga.

Kukiuka sheria ya sharia

Huko Hiran, al-Shabaab imekuwa ikitoa amri ambazo hazina uhusiano na sharia hivyo wanachama wake wanaweza kuepukana na ujambazi na uasherati, alisema mkuu wa poilisi wa Hiran kanali Isaaq Ali Abdullahi.
Majaji wa Al-Shabaab hawaelewi kikamilifu falsafa ya sheria ya kiislamu na kanuni za msingi za mfumo wa sheria wa haki na usiopendelea, alisema. Uamuzi wao sio halali kwa sababu unachochewa kisiasa, una kisasi na kuzingatia mfumo wa sheria wa kula njama, alisema.
Abdullahi aliishutumu al-Shabaab kwa kumkata kichwa mzee mwanaume na kijana wa kiume tarehe 22 Mei huko Dudumo Qaris, kilometa 45 kaskazini magharibi mwa Beledweyne. Wapiganaji pia waliiba dazeni za ngamia kutoka vijijini, alisema.
"Muda umefika kuwasaka hao wasaliti kutoka al-Shabaab, ambao wanahusiana na al-Qaeda, na kuwaondoa kutoka katika miji mbalimbali na vijiji katika mkoa ili kukomesha uonevu, ukandamizaji, ubaguzi na kudharau [raia]," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Tumefikia katika hali ambapo tunahitaji kutambua matamanio yetu, kwa sababu hivi karibuni utambuzi wa uhuru utakuwa kwetu, ambao watu wetu wanastahili kwa sababu ya kujitoa kwa kiasi kikubwa," alisema.
Ahmed Abdullahi Osman Inji, aliyekuwa kaimu mkuu wa usalama wa Hiran, alisema waathirika wawili walikuwa mjomba wake mwenye miaka 90, Hussein Aadan Toore, na mtoto wa kiume wa Toore. Wauaji waliwakata vichwa kwa kutumia jambia kali na kuwaacha kuvuja damu hadi kifo.
Muda wowote utakaochukua, al-Shabaab siku moja watapigwa na viongozi wao watatakiwa kwenda mbele ya mahakama ya kijeshi kujibu makosa ya gizani, alisema Inji.
"Ulipuaji wa mabomu na ukataji vichwa hauwezi kuendelea," alisema Inji. "Vikosi vya serikali vinachelewa kutekeleza operesheni zao za kijeshi kuzuia njia [za al-Shabaab] zisizo na heshima zinazosababisha maumivu na ugumu kuhusu watu wa Somalia, ambao walilazimishwa kumeza machungu ya mateso na kunyimwa maisha ya kisasa."

DK. HOSSEAH WA TAKUKURU AFUNGUKA, ASEMA TAKUKURU INATENGWA NA SERIKALI.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah 

Dodoma. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, amefunguka na kueleza sababu za taasisi yake kushindwa kuwakamata walarushwa wakubwa kwa kuwa Serikali imemfunga mikono.
Akitoa majumuisho katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa nchini (APNAC) jana, Dk Hoseah alisema kuwa Serikali imeitenga Takukuru na kuwafanya waishi kama yatima.
Huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge, mkurugenzi huyo alisema kuwa amekuwa akishangazwa na lawama ambazo amekuwa akibebeshwa kila wakati kuwa ameshindwa kumaliza rushwa wakati bila kuziangalia sheria.
“Mnanipa lawama kila wakati, lakini huwezi kuanzisha chombo kama Takukuru halafu ukamfunga mikono mhusika, na mimi mmenifunga mikono nifanyeje jamani? Alihoji na kuongeza:
“Hata katika rasimu ya Katiba bado mmetutenga kama watoto yatima, wenzetu wote mmewaweka tena hata CAG mmesema kuwa mamlaka yake akiteuliwa basi asiingiliwe wala kuhojiwa…mamlaka gani mtu asihojiwe jamani, mimi nikiuliza Takukuru mnasema subirini Serikali ya Tanganyika.”
Gazeti la Guardian la Uingereza la Jumapili ya Desemba 19, 2010, lilitoa taarifa ya siri kuhusu wala rushwa wakubwa kulindwa Tanzania. Gazeti hilo lilichapisha taarifa za mtandao wa WikiLeaks uliokuwa ukimilikiwa na mwandishi wa habari wa Australia, Julian Paul Assange, ukimnukuu Dk Hoseah.
Dk Hoseah alinukuliwa na WikiLeaks akimueleza mwanadiplomasia wa Marekani aitwaye Purnell Delly, Julai 14 jijini Dar es Salaam mwaka 2007 kuhusu uwezo na nia ya Rais Kikwete katika kushughulikia ufisadi.
Alidai Rais Jakaya Kikwete alikuwa anakwamisha kuchunguzwa kwa vigogo wa Serikali wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, na pia anahofia maisha yake kama mkuu wa Takukuru. Hata hivyo, Dk Hoseah kwanza alikiri kukutana na ofisa huyo ofisini kwake Julai 2007, lakini alikanusha kuzungumza kuwa Rais Kikwete alikuwa hataki sheria ichukue mkondo wake katika kuwachunguza vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa.
Atoa ushauri kwa Serikali
Kwa mara ya kwanza jana kiongozi huyo aliitolea uvivu Serikali kuwa imekuwa ikichangia mambo mengi katika rushwa ikiwamo usiri mkubwa katika rasilimali za nchi.
“Lazima Serikali iwe wazi, huwezi kuwaficha wananchi rasilimali zao eti ni siri kwa sababu ya sera mbovu, tunawaambia wananchi watanufaika na mirabaha ya asilimia tatu hiyo siyo sahihi jamani ndiyo maana tunashindwa kutoa majibu kwa wananchi wetu hilo ni tatizo jingine linalosababisha mambo ya rushwa,”alisema na kuongeza: “Siyo kila jambo ambalo serikali inapewa ushauri ni baya.”
Alipinga kitendo cha viongozi kuwa na kigugumizi katika uwajibikaji na akataka itungwe sheria kali ya kutaka kiongozi awajibike mara anapokuwa ametuhumiwa kwa jambo lolote aachie ngazi na kupisha uchunguzi kama ilivyo kwa nchi zingine.
Credits; Gazeti la Mwananchi

ELIMU YA NAMNA YA KUEPUKA RUSHWA KWA SEKTA YA AFYA WILAYANI NACHINGWEA.

Wadau wa sekta ya Afya toka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Nachingwea wakiwa katika majadiliano ya njia za kujiepusha na adui rushwa hivi karibuni, mafunzo haya yalitolewa katika ukumbi wa TRC mjini Nachingwea na maafisa wa TAKUKURU(hawapo pichani).

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uuguzi Nachingwea wakisikiliza maelekezo ya Maafisa wa TAKUKURU  juu ya mapambano dhidi ya rushwa na uundaji wa Klabu za Wapinga Rushwa Vyuoni na mashuleni.

Jumapili, 9 Juni 2013

ELIMU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA YATOLEWA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WILAYANI NACHINGWEA.

Afisa wa TAKUKURU Bw. Hassan Omari wa Nachingwea akipokea risala toka kwa kiongozi wa Klabu ya Wapinga wa Rushwa shule ya sekondari Marambo wakati wa ziara ya uhamasishaji wa mapambano dhidi ya rushwa hivi karibuni.

Baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari Marambo huko Nachingwea wakisikiliza mawaidha toka kwa maafisa wa TAKUKURU(hawapo pichani).

WANAUSHIRIKA WA RWANGWA, NACHINGWEA NA LIWALE WADHAMIRIA KUUNDA CHAMA KIKUU KIPYA CHA USHIRIKA CHA RUNALI BAADA YA AZIMIO LA KUJITOA ILULU.

Naibu Waziri TAMISEMI Mh. Majaliwa(Mb) akihutubu katika mkutano wa viongozi wa vyama vya  ushirika vya msingi toka Liwale, Rwangwa na Nachingwea ulioazimia kwa pamoja kujitoa toka chama kikuu cha Ilulu na kuunda RUNALI. Mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea hapo juzi.

Wajumbe tisa toka vyama tofauti waliopewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuunda  chama kikuu kipya cha RUNALI kinachotarajiwa kuwa kimesajiliwa mapema kabla ya msimu ujao wa ununuzi wa korosho, mkutano huu wa mageuzi haya ulifanyika jana juzi tarehe 07/06/2013.(Picha kwa hisani ya Lindi Yetu Blog)

HONGERENI TIGO KWA KUZINDUA INTERNET YA SPIDI KUBWA WILAYANI NACHINGWEA. MMEKUWA WA KWANZA KATIKA KILA JAMBO LENYE NAFUU KWA WATANZANIA, NAJUA WENGINE WATAIGA MFANO WENU.

Jumapili, 2 Juni 2013

WATU WATATU WAMEPOTEZA MAISHA HUKO PEMBA BAADA YA KUANGUKIWA NA TANKI LA ZEGE WALILOKUWA WANALIBOMOA LEO ASUBUHI.

Picture
Wananchi wakiuangalia mnara wa tangi la maji ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi watatu leo asubuhi

BREAKING NEWS TOKA RADIO ONE STEREO NI KUWA MELI YA MV BARUATI INATEKETEA KWA MOTO KATIKA BANDARI YA TANGA HIVI SASA. MELI HIYO NI YA MIZIGO INAYOFANYA SAFARI ZA TANGA, ZANZIBAR, DAR NA MTWARA.

 

MREMBO AANIKA MAKALIO MBELE YA WATU ALIPOMKUMBATIA MSANII OMMY DIMPOZ MAJUZI HUKO TABORA.

Mrembo ambaye hakufahamika jina lake alitoa kali ya mwaka alipoonesha makalio yake bila kujali mbele ya halaiki ya watu katika kinyanga'nyiro cha kumsaka Miss Redds Tabora 2012 hivi karibuni.
Naamini pombe au kilevi chochote hupelekeawatu kujisahau na baadae kujuta wanaposituka na kuambiwa mambo waliyoyafanya, Watanzania tuchunge maadili yetu.
Picha kwa hisani ya  bataboiz