Jumatatu, 29 Julai 2013

JIPYA TOKA TRA; MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI ZA MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO.

 
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mamlaka hiyo Bw. Ramadhani Sengati.


Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia)akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.


Meneja wa Mradi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ramadhani Sengati akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua jinsi gani mfumo huo utaleta tija hasa katika ukusanyaji wa kodi, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari, kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka hiyo Bw. Richard Kayombo.
(Picha zote na Hassani Silayo)




ISO 9001: 2008 Certified

MFUMO MPYA WA KULIPA ADA ZA MWAKA ZA MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO
Kuanzia mwezi Agosti 2013 malipo yote ya ada za mwaka za magari (annual road license) yatafanywa kwa njia ya mtandao kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.

Hii inatokana na maboresho ya mifumo ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kuyafanya ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Benki Kuu.
Mfumo huu utatumika kulipa ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa.

Faida za mfumo.
Mfumo huu umeanzishwa kutokana na faida nyingi kama:
  • Mfumo huu ni rahisi kutumia na utapunguza misongamano isiyo ya lazima katika ofisi za Mamlaka ya Mapato na benki na hivyo kumwezesha mlipakodi kulipa ada ya gari lake akiwa mahali popote nchini.
  • Mfumo huu una panua wigo wa njia za kulipa kodi kwahiyo unampa mlipakodi uhuru wa kuchagua njia ambayo anaona ni rahisi kutumia kutokana na mazingira atakayo kuwamo.
  • Vilevile kwa kutumia utaratibu huu mlipakodi anaweza kuhakiki kiwango cha ada ya gari anachotakiwa kulipa na hivyo kuepuka udanganyifu unaofanywa na vishoka ambao huwarubuni wananchi kwa kuwapa taarifa za viwango vya ada za magari visivyo sahihi.
  • Mfumo huu ni salama kwani kuna uhakika kwamba malipo yote ya kodi yanakwenda Benki Kuu kwani unaondoa mwingiliano wa wafanyakazi wa TRA na walipakodi.
  • Kwa upande mwingine mfumo huu unaiwezesha TRA kukusanya kodi kwa gharama nafuu.
Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari ni kama ifuatavyo:
  1. Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za  gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.  
  2. Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
  3. Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
  4. Kuchukua cheti: (sticker ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya TRA ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyoitumia kufanya malipo.
Zingatia.
Ili kuweza kuchukua kadi ya gari mlipakodi anatakiwa kuwa na kitambulisho chochote kama vile kitambulisho cha Taifa, Hati ya kusafiria, Lesseni ya udereva, Kitambulisho cha mpiga kura n.k.

Mfumo wa kulipa ada za magari za mwaka ni muendelezo wa maboresho ya mfumo wa kulipa kodi kwa mtandao (Revenue Gateway)  ambao ulibuniwa na TRA kwa kushirikiana na Benki Kuu (BOT). Mfumo huu umeanza kutumika rasmi Julai Mosi 2013.
Mfumo wa RG pamoja na kuwa unaunganisha mifumo ya TRA na Benki Kuu pia unaiunganisha TRA na walipakodi, Benki za Biashara, Makampuni ya simu (M-PESA, TIGOPESA, AIRTELMONEY n.k) pamoja na wadau wengine kama vile Hazina na NIDA.

Wito.
Tunatoa wito kwa wananchi wote kuungana na TRA katika maboresho ya mifumo yanayoendelea kwa kuitumia mifumo hiyo kwani imewekwa kwa ajili yao ili waweze kulipa kodi stahiki bila usumbufu wowote.
Pia tunawaomba wananchi wote wanaolipa ada mbalimbali za magari kuitumia fursa hii ya kulipa kwa njia ya mtandao ili waweze kuendelea vema na shughuli za ujenzi wa taifa badala ya kutumia muda mwingi katika misurusu kwenye mabenki.
PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU

RICHARD M. KAYOMBO
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA
S.L.P 11491
Dar es salaam
Simu: 2119343
Simu za bure; 0786 800800, 0713 800 333, 0800110016

Jumapili, 28 Julai 2013

KONGAMANO LA WANATAALUMA LINAENDELEA HIVI SASA UKUMBI WA NKRUMAH CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM; WATOA MADA WAJIELEKEZA KATIKA MUSTAKABALI WA AMANI NA USALAMA WA TAIFA LETU KWA MIAKA HAMSINI IJAYO.

Profesa Bernadeta Killian Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa mada yake leo katika Ukumbi wa Nkrumah kuhusu Mustakabali wa Amani na Usalama wa Taifa letu kwa miaka hamsini ijayo. Profesa amesema njia kuu ya kuelekea kwenye Amani ni Amani yenyewe. Hongera kwa Profesa kwa kutoa mada nzuri isiyo na upendeleo kwa hadhira yake.
 
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada kwa makini toka kwa Wachokoza Mada.

Profesa Killian akiendelea kuchokoza mada yake iliyosema nini dhima ya siasa katika kujenga au kuharibu amani ya Tanzania(Picha kwa hisani ya ITV)
 

VIDEO TOKA KTN; JAMAA ALAUMU BARRACK OBAMA KUTOTEMBELEA KENYA.

Huyu jamaa wa jirani hapo Kenya alitoa maoni yake juu ya ziara ya Rais Barrack Obama na kulaumu sana kwa nini hakutembelea nchi yao na badala yake Tanzania, hebu tumsikilize na tuone watu tulivyokuwa wabinafsi kila sehemu.

Alhamisi, 25 Julai 2013

SUAREZ ANAKARIBIA KUTUA ARSENAL HIVI KARIBUNI.

For all his gifts as a footballer, subtle communication has never been Luis Suarez’s forte. Just ask Patrice Evra or Branislav Ivanovic about that.

Nevertheless, as he seeks to leave Liverpool this summer, the club’s Uruguay forward is at least deserving of an audience.
Suarez, of course, is one of the Barclays Premier League’s pantomime villains. The words the FA found him guilty of uttering to Evra almost two years ago and the attempt to bite a chunk out of Ivanovic’s arm last season have made sure of that.

Saying his goodbyes? Luis Suarez has made no secret of his desire to leave Liverpool
Saying his goodbyes? Luis Suarez has made no secret of his desire to leave Liverpool
He is also an exceptionally talented footballer. Without his goals last season, Liverpool’s campaign would have ground to a halt long before their eventual seventh-place finish.
No wonder, then, that Suarez has spent much of the summer wondering if his career is about to head down a blind alley at Anfield.
The disingenuous nature of Suarez’s comments when seeking to explain his discontentment has been irksome. By claiming he has been persecuted by the English media, Suarez has invited ridicule.
This should not be allowed to mask the real issue here — and that is that Liverpool do not look like a club capable of giving the 26-year-old what he needs or wants on the field.
To put it bluntly, Suarez is a first-rate centre forward, comparable with all but the very best.

World class: But for all of his talent Suarez doesn't appear to be happy
World class: But for all of his talent Suarez doesn't appear to be happy


Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2376858/Liverpools-Luis-Suarez-right-want-leave-Anfield.html#ixzz2a0Y0A2hC

Jumatatu, 22 Julai 2013

PICHA YA LEO; HELIKOPTA IKIWA IMEBEBA RADA HUKO NACHINGWEA LEO MCHANA, WANASEMA ETI INAFANYA UTAFITI WA MADINI.

Leo hapa Nachingwea mjini nilibahatika kuona Helikopta ikiruka ingawa kwa mbali ikiwa imebeba rada chini yake na mwendo wa wastani, wenyeji waliniambia inafanya utafiti wa madini ili kujua yapo mahali gani, jamani Nchi yetu yaelekea imebahatika kuwa na mali nyingi lakini wageni ndio wanaonekana wana elimu hiyo na wanafaidika wao, Viongozi tuwe makini.

Jumapili, 21 Julai 2013

WANAJESHI WALOFIA DARFUR MIILI YAO IMEREJESHWA JANA JIONI,RIP MASHUJAA WETU.


Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya kuondolewa katika uwanja wa jeshi.

Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya kuondolewa katika uwanja wa jeshi.