Jumamosi, 31 Agosti 2013

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO MBALIMBALI NCHINI.

Ili kupata majina bofya katika sehemu ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika chuo husika.

UDSM




MZUMBE 

 
 SAUT
WANAFUNZI 2013/2014

TEKU
WANAFUNZI 2013/2014

TUMAINI MAKUMIRA:

 Bofya hapa 

SERIKALI YA MAREKANI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAWASILIANO KWA JWTZ NA POLISI HAPO JANA.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Marekani pamoja na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi.


Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt akitoa hotuba yake kabla ya uzinduzi wa mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Wakwanza kutoka kulia (aliyekaa) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini.


Baadhi ya vifaa vya mawasiliano vilivyozinduliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi pamoja na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt. Vifaa hivyo vya mawasiliano vitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 

MWENYE BAHATI HABAHATISHI, MZEE GURUMO ATIMIZA NDOTO ZAKE ZA KUWA NA GARI, DIAMOND AMPATIA GARI MZEE GURUMO.


AKIMKABIDHI MZEE GURUMO GARI LA THAMANI YA MILIONI SITA.


KATIKA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA NUMBER ONE, DIAMOND ALIMZAWADIA GARI MZEE GURUMO ALIYESTAAFU MUZIKI HIVI KARIBUNI.

Alhamisi, 29 Agosti 2013

KIFAA CHA LIVERPOOL, DANIEL STURRIDGE.

Trademark: Sturridge celebrates his second goal against Notts County
Trademark: Sturridge
 
Groove: Anfield watches Sturridge's dance celebration
Daniel akisherehekea ushindi kwa kucheza dansi.

TANZIA; MWANAJESHI WA TANZANIA MEJA KHATIB MSHINDO AMEFARIKI DUNIA KWA KUSHAMBULIWA NA WAASI WA M23 WA KONGO.




JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo  : “N G O M E”                                             Makao Makuu ya Jeshi,


Simu ya Mdomo  : DSM  22150463                                         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                                       DAR ES SALAAM,   29  Agosti, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                  
TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC,GOMA

1.       Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO.

2.       Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3.       MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.


Dar es Salaam

Jumatano, 28 Agosti 2013

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA GESI YA MTWARA UNAENDELEA KWA KASI.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akikagua mtambo maalumu kwa ajili ya kuunganisha bomba ambao kwa hivi sasa upo katika kijiji cha Somangafungu wilayani Kilwa.

Baadhi ya mitambo ya kisasa inayotumika katika kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kama ilivyokutwa ikisubiri kuanza kazi katika kijiji cha Somangafungu Wilayani Kilwa.

Mitambo maalumu ikiandaliwa kwa ajili ya kuweka mitambo itakayotumika kuwekea zege mabomba ya kusafirishia gesi asili kutoka kina kirefu baharini. 
(Picha zote na Mohamed Saif)