Jumapili, 26 Januari 2014

MLIPUKO WA GHALA LA SILAHA WAUA ISHIRINI HUKO KONGO DRC


Uharibifu uliotokana na mlipuko

Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghala la silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo ,vimesema kuwa nyumba nyingi zilaharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.

Kwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco,zaidi ya watu 50 pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radi
Lengo la Monusco nchini humo ni kupokonya makundi yanayopigana silaha. DRC inajaribu kutokamana na vita vilivyosababisha mamilioni ya vifo kati ya mwaka 1998 na 2003.
'Nimewaamrisha maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi hicho cha Monusco.
Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi.bbc

Jumamosi, 4 Januari 2014

MAREHEMU MGIMWA KUZIKWA JUMATATU HUKO IRINGA.

Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa, ambaye alifariki siku ya Jumatano kwa sababu za kawaida katika hospitali moja huko Afrika ya Kusini, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu (tarehe 6 Januari), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.

Marehemu William Mgimwa.

Mwili wa Mgimwa unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, William Lukuvi.Mgimwa alifariki katika hospitali ya Mediclinic Kloof ya Pretoria baada ya kulazwa kwa matibabu ya dharura. Mwezi huu angetimia miaka 64.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Mh. William Lukuvi(Mb)
Siku ya Jumapili, mwili wa Mgimwa utapelekwa Ukumbi wa Karimjee, ambako maafisa na wananchi watatoa heshima zao za mwisho, ikifuatiwa na sala maalumu, Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari.
Mgimwa, mkongwe wa Benki ya Taifa ya Biashara ya Tanzania, alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 na kuteuliwa waziri wa fedha mwaka 2012 na ilisifika kwa kuongoza jitihada za Tanzania za kutafuta masoko ya dhamana ya kimataifa ili kugharamia uwekezaji na kukabiliana na umaskini, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP