Ijumaa, 11 Desemba 2015

RAIS MAGUFULI AMETANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LEO....

Picha za Rais Magufuli akielekea kutangaza baraza la mawaziri leo

mg5
mg5Kuelekea ukumbi wa mikutano Ikulu.
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametangaza baraza la mawaziri December 10 2015 ambapo hata hivyo hajamaliza kutaja mawaziri wengine akisema anaangalia ni nani wa kumuweka kwenye hizo wizara zilizobaki
mg3
mg7
mg7Picha ya pamoja na Waandishi wa habari
mg6
Rais Magufuli, Katibu mkuu kiongozi Sefue, Waziri mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Picha zote ni kutoka Ikulu.

Ijumaa, 20 Novemba 2015

WAZANZIBAR WAISHIO UINGEREZA WAANDAMANA KUPINGA KUSITISHWA KWA UCHAGUZI ZANZIBAR...

Maandamano ya wazanzibari London/UK

maandamano5
Baadhi ya picha zikionesha Wazanzibar waishio sehemu mbalimbali za Uingereza wakikusanyika mtaa wa Downing ambako ndiko ziliko ofisi za Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon kupeleka barua ya malalamiko juu ya namna wasivyoridhika na Uchaguzi ulivyoghairishwa huko nyumbani Zanzibar.. Maandamano hayo yalifanyika jana huku kukiwa na hali ya manyunyu ya hapa na pale lakini bila kujali watu walimiminika mitaani...

Jumamosi, 14 Novemba 2015

RAIS MAGUFULI APATA MSIBA WA MJUKUU WAKE HAPO JANA...

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika janaNov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,jana Nov 13, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, jana Nov 13, 2015.

Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,jana Nov 13, 2015.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,jana Nov 13, 2015.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,jana Nov 13, 2015.
Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika jana Kimara, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, jana Nov 13, 2015. 
Picha na OMR

Ijumaa, 23 Oktoba 2015

MAHAKAMA KUU LEO IMEAMUA KUKAA MITA 200 AU ZAIDI BAADA YA KUPIGA KURA HAIRUHUSIWI...


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa uamuzi wa mvutano wa kukaa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia kura na kusema kuwa haruhusiwi mtu yeyote kukaa hata kwenye umbali zaidi ya mita hizo.

Jumapili, 4 Oktoba 2015

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA AMEFARIKI ALFAJIRI YA LEO BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI.

 Marehemu Mtikila alikuwa akitokea mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam kwenye shughuli zake akiwa na gari dogo na watu wengine watatu na gari ilipata ajali majira ya saa 10 alfajiri ya leo. Mchungaji alifariki hapohapo na wenzake wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali. Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. 
Marehemu Mtikila akiwa eneo la ajali. Marehemu atakumbukwa katika harakati zake za kupigania Taifa la Tanganyika, Mgombea binafsi na haki nyingine nyingi za Binadamu. Mwenyeezi Mungu amlaze mahali pema peponi Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila.

Jumapili, 6 Septemba 2015

RATIBA YA KAMPENI WAGOMBEA URAIS VYAMA NANE TIZAMA HAPA CHINI.

WAKULIMA WA MIKOA YA LINDI, MTWARA NA PWANI CHANGAMKIA FURSA YA KUKODI MATREKTA KWA BEI NAFUU MSIMU HUU WA KILIMO..




TUNAKODISHA TREKTA!!
"Kwa wale wakulima wenye ekari za kutosha maeneo kuanzia Mkuranga, Mwarusembe, Kimanzichana ya Mkiu, Mkamba nk. hadi maeneo ya Ikwiriri na Rufiji.... Lakini pia kama kuna maeneo ambayo tunaweza kukodishwa kwa ekari 100 na kuendelea sisi tutajipanga nakukufikia…. Haijalishi ni udongo wa aina gani, trekta yetu ina nguvu za kupambana na hali zote za udongo!!
 
Mkombozi wa ukweli kapatikana sasa. Ile hofu ya kulima kwa muda muafaka imepata jawabu!!
Tumeleta trekta linalofaa kupambana kwa kazi maeneo hayo, trekta hilo ni FORD 7500.
Bei zetu ni nzuri zipo baina ya Tshs. 40,000/= hadi 60,000/= kulingana na umbali.
Kwa mawasiliano:
1. 0787519910 na 0767519910... Tutakujibu kwa simu na sms!!
2. Kwa 0787519910 tutakujibu kwa whatsapp
4. Tembelea pia blog yetu moddyrajabu.blogspot.com