Jumanne, 30 Juni 2015

PICHA YA LEO; UNAMKUMBUKA MWANAMUZIKI SAMANTA MUMBA TOKA MAREKANI.....!!?

Bouncing back: The star, who is based in LA, looked happier and healthier than everBody II Body: Samantha couldn't get enough of her police officer hubby's kisses


True love: Samantha showed her affection for her American husband Torray Scales as they kissed in the sea
Samanta akiwa ufukweni na mumewe...
Lucky escape: The 31-year-old singer was recently involved in a car crash, but emerged uninjured
Torray Scales, mume wa Samanta....
Akiwa na umri wa miaka 33 Samanta bado anang'aa. mwezi machi mwaka 2015 walipata mtoto wao wa kwanza katika ndoa ilyofungwa 2012.

HUKUMU YA KESI YA MAWAZIRI WA MKAPA KUTOLEWA TAREHE 03/07/2015

MGONJA, YONA NA MRAMBA
HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu.
Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya kutokuwepo Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo. Mahakimu wengine wanaoongoza jopo hilo ni Jaji John Utamwa na Jaji Sam Rumanyika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji John Utamwa leo ni kwamba Hakimu Kinemela yupo mkoani Dodoma kwa shughuli maalum za kibunge na anatarajia kurejea jijini Dar kati ya kesho au keshokutwa, hivyo hawawezi kutoa hukumu hiyo bila jopo hilo kukamilika.
Credits;globalpublishers